Unknown Unknown Author
Title: PICHA;MAANDALIZI YA NASSARI KUFUNGA NDOA KESHO YAIVA:WAJUE BAADHI YA WABUNGE WA CHADEMA AMBAO HAWAJA OA MPAKA LEO HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
  NDOA YA NASSARI, HALIMA MDEE YAOTA MBAWA, JAMAA ANAOA KESHO! Joshua Nassari na Halima Mdee, mwaka 2012 Na Mwandishi wa brothe...

 

NDOA YA NASSARI, HALIMA MDEE YAOTA MBAWA, JAMAA ANAOA KESHO!

Joshua Nassari na Halima Mdee, mwaka 2012

Na Mwandishi wa brotherdanny5.blogspot, Meru

UWEZEKANO wa kuwepo kwa ndoa baina ya mbunge kijana wa Chadema wa jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, na Mbunge wa Jimbo la Kawe (Chadema), Halima Mdee, umeota mbawa baada ya taarifa kubainisha kwamba Nassari sasa anatarajia 'kuvuta' jiko kesho katika kanisa moja huko Arumeru.
Mdada ambaye ameuvutia moyo wa Nassari ametajwa kwa jina na Anande Nko, na kwamba jana ndiyo ilikuwa 'Send Off' yake tayari kwa tukio kubwa la harusi.
Mahaba baina ya Nassari na Halima Mdee yalidaiwa kuchomoza mwaka 2012 wakati ule mbunge huyo akiwa ameteuliwa kuwania ubunge katika uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha mbunge wa jimbo hilo, Jeremiah Solomon Sumari, ambaye pia alikuwa naibu waziri wa fedha.
Wakati wa kampeni zake, taarifa zilizagaa kwamba moyo wa Nassari ulikuwa umemdondokea Mdee na yeye mwenyewe hakuweza kulificha hilo.
Nassari alitangaza ndoa yake na Halima Mdee katika kipindi chote cha kampeni na hata baada ya uchaguzi mdogo wa ubunge wa jimbo lake mwezi Aprili mwaka 2012. 
Wachunguzi wa masuala ya siasa mkoani hapa wanasema hii pia ni mbinu mojawapo ya kujiandaa na kinyang’anyiro cha kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.
Katika uchaguzi uliopita, Nassari alipata shida kubwa sana kutoka kwa wapinzani wake waliodai kuwa kwa sababu ni kapera isingekuwa jambo la busara kwa wananchi wa jimbo hilo kumchagua.
Hatua hiyo ilisababisha mbunge huyo kuamua kumtangaza hadharani Mdee kama mchumba wake ambaye wangefunga naye ndoa mara tu baada ya kumalizika uchaguzi mdogo wa jimbo hilo.
Hata baada ya ushindi wake, Nassari aliendelea kumnadi Halima Mdee kuwa ni mkewe mtarajiwa na anatarajia kufunga ndoa kubwa sana ambayo nayo ingeweza kuhudhuriwa na viongozi wa kitaifa kutoka ndani na hata nje ya Chadema.
Lakini baada ya uchaguzi huo mdogo kupita bado Nassari hakuweza kuizungumzia ndoa hiyo hali ambayo ilifanya wananchi wa jimbo hilo kubaki na mshangao.
Jitiada za kumpata mbunge azungumzie suala hilo ziligonga mwamba blogu hii kuwasiliana kupitia simu yake ya kiganjani na yeye kusema kwamba yuko kwenye kikao.
Aidha, blogu hii ilimtafuta Halima Mdee, lakini simu yake ya kiganjani haikuweza kupatikana.

Hii hapa ni habari iliyopamba magazeti Aprili 16, 2012:

MBUNGE wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) amesema sasa yuko tayari kufunga ndoa na Mbunge mteule wa chama hicho wa Jimbo la Arumeru Mashariki, Joshua Nassari. 

“Nafurahi kwamba Nassari hatimaye ameshinda ubunge katika uchaguzi mdogo,” alisema Mdee wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha na Meru juzi katika viwanja vya Leganga kusherehekea ushindi wa chama chake katika uchaguzi huo. 

Mdee alifafanua, kwamba yeye na chama chake walikuwa wamebanwa na kampeni za kuhakikisha Chadema inatwaa jimbo la Arumeru Mashariki na ndiyo sababu hakujibu mara moja maombi ya Nassari ya kumwoa aliyoyatoa katika moja ya mikutano yake ya kampeni. 

“Naondoka kwenda Dar es Salaam kujiandaa kwa Mkutano ujao wa Bunge, kisha nitakwenda Dodoma ambako nitamsubiri Nassari na kwa pamoja tutafanya maandalizi,” alisema Mdee huku akishangiliwa na hadhira hiyo huku wakiimba na kucheza katikati ya mvua iliyokuwa ikinyesha. 

Mdee alisema ndoa kati ya wabunge hao wawili wa Chadema ni wazo zuri na itatangazwa sana na kuandika historia. 

Alipoona anashambuliwa sana na wapinzani wake juu ya useja wake katika kampeni hizo, Nassari hatimaye alitangaza kumwoa Mdee ambaye pia hajaolewa. 

Na katika moja ya mikutano ya hadhara, alisimama naye jukwaani kukampeni. 

“Kuna viongozi wengi wa kidini Dodoma, ikiwa ni pamoja na ndani ya Bunge ambao watatushauri jinsi ya kulitimiza hili,” alisema Mdee na kuongeza kwamba baba yake Joshua, Mchungaji Samuel Nassari alipata kusema, ‘mwanamke mzuri ni zawadi kutoka kwa Mungu’. 

Chadema ina idadi kubwa ya wabunge vijana ambao hawajaoa, ikiwa ni pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Mr Sugu’; wa Ubungo, John Mnyika; wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe na sasa Nassari. 

SOMA ZAIDI.....
 

JOSHUA NASSARI (MB) KUFANYA HARUSI YA ALAIKI KESHO JIMBONI KWAKE


Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa amekumbatiana na Mchumba wake Bi Anande Nnko muda mfupi baada ya kumtafuta kwa muda katika sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwa Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Bi ,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru.


Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.

Kwa Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana  watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.


"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.

Na ssari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .
Na Michuzi Media Group
MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top