Timu ya Taif ya mpira wa miguu Taifa Stars na Tanzania kwa ujumla
imepanda nafasi 9 juu katika ubora wa viwango vya mchezo huo Dunia baada
ya kufanya vizuri katika michezo ya kimataifa ya hivi karibuni ikiwemo
ya kirafiki pamoja na ya kusaka nafasi ya kushiriki fainali za kombe la
mataifa ya Afrika mwakani nchi Morocco.
Viwango hivyo vimetolewa jana na Shirikisho la Mpira wa miguu ulimwenguni FIFA ikiwani takwimu za mwisho kutolewa na shirikisho kabla ya kuanza kwa fainali za kombe la Dunia zinazo tegemea kuanza kutimua vumbi Juni 12 nchini Brazil.
Tanzania sasa imekuwa katika nafasi ya 113 Duniani baada ya kupanda na kuchomoka katika nafasi ya 122 ilipo kuwa kabla ya takwimu za jana.
Kwa viwango hivyo sasa Tanzania itakuwa nafasi ya 3 katika ukanda wa Afrika Mashariki ambapo Uganda inaongoza ikiwa katika nafasi ya 86 ikifatiwa na Kenya katika nafasi 108 duniani.
Kwa upande wa Afrika nzima inaongoza Algeria inaongoza katika nafasi ya kwanza Afrika huku Dunia ikiwa katika nafasi ya 22 ikifatiwa na Ivory Coast ambayo ni ya pili Afrika na Duni ikishika nafasi ya 23.
Hispania inaongoza Dunia kwa ubora ikifatiwa na Ujerumani na Brazil katika nafasi ya 3 huku Ureno ikishika nafasi ya 4 na Argentina ikifunga mlango wa 5 bora za viwango vya ubora katika mpira wa miguu Duniani kote.
MJUMBE Sr

Post a Comment