Baada ya kuwa katika machafuko ya muda mrefu hatimaye nchi ya Ukraine imepata Rais mteule ambaye ni Petro Poroshenko. Bwana Poroshenko ambaye anatarajiwa kuapishwa rasmi kama kiongozi wa taifa hilo hilo amesema kuwa mazungumzo mengine na Urusi yatafanyika hapo kesho siku ya Jumapili.
Amepongeza mkutano wake na rais wa Urusi Vladmir Putin kama mwanzo wa majadiliano kuhusu mzozo unaondelea mashariki mwa Ukraine.
Hata hivyo mapigano yaliendelea Ijumaa huku waasi wanaounga mkono Urusi, wakiripotiwa kudungua ndege ya serikali karibu na eneo linalodibitiwa.
Post a Comment