Unknown Unknown Author
Title: LEGAN MICHAEL:HARAKATI ZA KUDAI HAKI ZILINISIMAMISHA CHUO UDSM,STORI NZIMAINGIA HAPA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
KAULI YA BW; LEGAN MICHAEL · SASA IMEKUWA HISTORIA. 2010 - 2014 Baada ya mihangaiko, mateso,kusimangwa, na kejeli nyingi k...
KAULI YA BW; LEGAN MICHAEL · SASA IMEKUWA HISTORIA. 2010 - 2014 Baada ya mihangaiko, mateso,kusimangwa, na kejeli nyingi kwangu juu ya elimu yangu sasa yameisha na kuwa historia. Mwaka 2010 nilifanikiwa kujiunga na masomo ya elimu ya juu chuo kikuu cha Dar -es- salaam na kwa tarataibu za masomo nilitakiwa nihitimu shahada yangu ya kwanza mwaka 2013. Mipango hiyo haikufanikiwa kwa kuwa uvumilivu wa kuwa mtumwa wa masomo na nidhamu ya uoga ulisha pale nilipoanza harakati za kudai haki za wanafunzi kuanzia pesa za mafunzo kwa vitendo, fedha za kujikimu na fedha za ada kwa wanafunzi wanyonge walionyimwa na bodi ya mikopo. Kwa kiwango kikubwa harakati zilifanikiwa na wanafunzi wengi kufurahia matunda hayo kwani pesa ya mafunzo kwa vitendo ilianza kutolewa sawa kwa wote ikiwa ni tofauti na mwanzo, pesa ya kujikimu iliongezwa kwa 2500/= na waliokuwa wamekosa pesa za ada walipata. Wakati wanafunzi wenzangu wakiendelea kufurahia matunda hayo, sisi tuliongoza harakati hizo RUNGU LA TIMUA TIMUA LILITUKUMBA na zaidi ya wanafunzi 80 tulitimuliwa. Kipindi hicho nikiwa mwaka wa pili wa masomo yangu ndipo nilipo pokea barua ya kusimamiswa masomo kwa mda wa miezi 11, Sitasahau kwani wakati huo ulikuwa mgumu kwangu, watu wengi hawakuwa na mimi tena, wengine walionesha kuchukia kuliko mimi mhusika lakini hali ILIKUWA TOFAUTI KWA WAZAZI WANGU KWANI WALINITIA MOYO JAPOKUWA NAO WALIKUWA WAMEUMIZWA NA MAMUZI HAYO. Ila tofauti na baadhi ya wenzangu ambao wazazi wao hawakuwaelewa na wengine mpaka sasa hawaelewani nao tena. Wengi walinisema vibaya na wapo walio nipongeza kwa juhudi zangu za kutetea wanyonge na kutokubali kuonewa. Hatimaye leo nimemaliza mtihani wangu wa mwishoa kwa kukamilisha masomo ya shahada yangu....Shukrani za dhati kwa Mwenyezi Mungu, WAZAZI wangu, marafiki, ndg na jamaa kwa ukaribu na maombi yao. MJUMBE Sr

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top