Unknown Unknown Author
Title: KIKONGWE WA MIAKA 90 AKUTWA AMEJINYONGA JUU YA MTI NA MJUKUU WAKE -SHINYANGA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwanamke (kikongwe)anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 85 hadi 90 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani juu ya mti karibu ...


Mwanamke (kikongwe)anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 85 hadi 90 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya katani juu ya mti karibu na nyumba yake katika mtaa wa Busalala kata ya Kizumbi tarafa ya Shinyanga mjini katika manispaa ya Shinyanga.

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Longinus Tibishubwa amesema tukio hilo limetokea jana saa sita mchana.

Amesema mwili wa marehemu uligunduliwa na mjukuu wa kikongwa huyo aitwaye Asia Muhammed huku akiongeza kuwa chanzo cha tukio hilo bado kinachunguzwa.
CHANZO:KIBONAJORO

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top