James Foley alipotea tangu alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria yapata miaka miwili iliyopita.
Foley ambaye katika video hiyo amevalia magwanda ya rangi ya chungwa akiwa amepiga magoti anasikika akisema kuwa ''Ninawaomba ndugu jamaa na marafiki wangu wasimame na kuzuia adui wangu Serikali ya Marekani kwa ukatili wanaoendelea kutekeleza ndani ya Iraq.''Katika video hiyo mwandishi huyo wa kujitegemea anaonekana kuuawa na mtu anayemruhusu kutoa semi yake ya mwisho.
Mpiganaji mmoja wa kundi hilo akizungumza kwa kizungu anailaumu Marekani kwa kifo cha mwandishi habari huyo.
''Kila siku mnaposhambulia jamhuri ya kiislamu manadhuru maisha ya muislamu na hivyo tunachukua maisha yetu ili iwe onyo kwako (rais) Obama''
BBC SWAHILI
Post a Comment