Taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora ambayo ameitoa leo kwa Waandishi wa habari ni kuhusu ajali ambayo ilitokea jana Aug 19 majira ya saa 9 alasiri ambayo ilihusisha mabasi mawili.
Mabasi hayo ni AM Coach na Sabena ambapo chanzo cha ajali hiyo kimedaiwa kuwa ni mwendo kasi wa mabasi hayo,majeruhi wamelazwa kwenye hosptali ya rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete ambao jumla yao ni 75,waliopoteza maisha jumla 17 na 10 wametambuliwa.
Madereva wote wawili ni miongoni mwa watu waliopoteza maisha kwenye ajali hii ambayo ilitokea Aug 19 eneo la Mlogolo wilaya ya Sikonge Mkoani Tabora ambapo basi la Sabena lilikuwa likitoka Mbeya kuelekea Tabora na AM lilikua likitokea Mwanza kuelekea Mpanda.
Chanzo:Milard ayo.com
Post a Comment