Serengeti Fiesta Tanga imemalizika kwa stage kushambuliwa na zaidi ya wasanii 15 ambao kwa pamoja walitoa burudani kwa wakazi wa Tanga,Mara nyingi stage ya Srengeti Fiesta huwa inatawaliwa na ‘Sapraiz’ na Tanga nao walikutana nayo hii.
Wasanii Hawa mara nyingi huwa hawatangazwi ili kutoa nafasi kwa wewe mhudhuriaji kupata burudani ambayo hukuitegemea,Tanga walipata ujio wa Tunda Man na Abdul Kiba on stage ambao walipanda na kushangiliwa sana
Upande wa Tunda Man alipanda wakati Madee akiimba na upande wa Abdul Kiba alipanda wakati kaka yake Ally Kiba alipokuwa akiimbaKiukweli alishangiliwa sana na kutoa salaam zake kwa wakazi wa Tanga na ilikua poa sana.
Wasanii wengine waliopefom ni pamoja na Ally Kiba,Madee,Abdul Kiba,Dogo janja,Ommy Dimpoz,Kadja,Young killer,Mr Blue,Roma Mkatoliki,Ney wa Mitego,Stamina,Chegge na Temba na wengine wengi na pia kulikua na washindi wa ngoma Baikoko ya Tanga.
CHANZO:KIBONAJORO
Post a Comment