Unknown Unknown Author
Title: LHRC:WARIOBA USICHOKE KUPIGANIA HAKI YA WA TANZANIA KUPATA KATIBA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kituo cha sheria na haki za binadamu kimemshauri aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya, jaji joseph warioba kutoka...

Kituo cha sheria na haki za binadamu kimemshauri aliyekuwa mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni ya katiba mpya, jaji joseph warioba kutokata tamaa katika kupigania haki ya watanzania kupata katiba wanayoitaka.

Mkurugenzi wa utetezi wa kituo hicho wakili Harold Sungusia, amesema kinachoonekana sasa ni kwamba jaji warioba ameanza kukata tamaa ya kupigania haki hiyo kutokana na mwenendo wa bunge maalum la katiba ulivyoendeshwa ikiwa ni pamoja na kufuta mambo mengi muhimu ikiwamo usawa wa haki za binadamu.
 
Wakichangia mada  kuhusu maudhui ya katiba iliyopendekezwa na Bunge maalumu la katiba wakati wa jukwaa la mchakato wa katiba mpya lililoandaliwa na mtandao wa kufuatilia sera mwanza ( MPI ), baadhi ya viongozi wa asasi na mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali wamekosoa baadhi ya mambo yaliyomo kwenye rasimu ya katiba iliyopendekezwa.
Chanzo:Itv tz

Tuna shukuru kwa kututembelea!


Sasa Una weza Uka tutembelea Mtandaoni Moja kwa moja kwa kuandika MJUMBE BLOG kisha Ingia hapo!
Upate Picha,Taarifa,Habari na Matangazo kila mara.

©Mjumbe Blog Volunteers.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top