Maharusi Bwana Claud Kihindo na Bibi Rehema Kayange wakiwa Mbele ya Keki yao ya Ndoa.
Wakiwa wamesha Ibua ishara ya Kusisimua na yenye Kuamsha hisia ya Furaha baina yao na wageni waalikwa.
Keki ikiwa ina katwa kwa Mara ya kwanza kabisa na Maharusi wote kwa kusaidiana!
Bwana harusi Claud Kihindo akiwa Ame waacha Hoi Hata wasaidizi wake na kuamsha kicheko Ukumbini alipo sema
"Sasa hapa sita hitaji tena kutafuta kandiri/Kibatari ili nipate mwanga ndani ya nyumba yangu! Si muna ona
Mtoto mwenyewe alivyo Mweupe?"
Ni ile Juma mosi ya Octoba 04 2014,Kijijini Idunda,Njombe!
Kijiji kilipo zizima kwa nderemo vifijo na Furaha!
Ishara ya Kumpokea Mwali wao Rehema Kayange Baada ya Kuwekwa ndani na Bwana Claud!
MJUMBE BLOG tuna toa Pongezi za dhati ya mioyo Yetu na
Tuna WAOMBEA MAISHA MAPYA YENYE KHERI NA FANAKA TELE!
Claud Kihindo ni Nani?
Ni Mdau wa MJUMBE BLOG tangu enzi za kuandika makala kwenye Karatasi ili zichapwe kwenye gazeti la Chuoni Pale TEKU kati ya Miaka ya 2009/2011!
Huyu ndiye aliye nifungulia Mlango wa Bweni la Chuoni kwa Mara ya kwanza nilipo jiunga chuo kikuu!
Nakumbuka Usiku ule Nilikuwa na Kibegi Cha kuning'iniza mkononi na nilivaa Kisuruari cha kubana mwili! Ukijumlisha na Mwonekano wa mwili wangu kuwa Mdogo enzi zile Basi alini uliza
"Nawewe Umekuja kusoma"?
Nadhani alitegemea Chuo kikuu aone kipande cha Mwili na Suti kubwa Mabegi Mengi na Gari la Mizigo ikiingia pale! Lakini Haikuwa hivyo!
Ilikuwa Ni Kama Nipo kwenye Transist Nita fuata nguo na Mizigo mingine kumbe ndio Nime Tua mabegi!
Na ikawa Juma na ukawa Muhula Mwaka na Hata Siku ya Kutunukiwa Shahada ya Kwanza ikafika!
Nashukuru nime shuhudia Tukio Muhimu sana Maishani mwa Mr Kihindo!
©Mjumbe Blog Volunteers.
Post a Comment