Unknown Unknown Author
Title: PICHA:MOTO WA JIJINI ARUSHA UME TEKETEZA BIDHAA ZA SANAA "CURIOUS AND CRAFT"!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET wakiwa wameduwa...





Sehemu ya Wafanyabiashara wa SOKO la
bidhaa za utamaduni lijulikanalo kwa jina
la MT.MERU CURIOS & CRAFTS MARKET
wakiwa wameduwaa bila kujua la kufanya
mara baada ya Soko hilo kuteketea kwa
moto usiku wa kuamkia leo na kuunguza
bidhaa zote za wafanya biashara zililopo
katika soko hilo.Habari picha kwa hisani
ya woindeshizza blog
Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Magesa
Mulongo ameagiza uchunguzi wa kina
kufanyika kufuatia soko la
wafanyabiashara wa Vinyago na bidhaa
mbalimbali za kitalii la Maasai Market
kuteketea kwa moto.
Mulongo ambaye alifatana na kamati ya
Ulinzi na Usalama alishangaa kuona
maduka hayo ambayo yapo jirani na Kikosi
cha Zima Moto kushindwa kuzima moto na
kusababisha hasara kwa wananchi.
"Sitakubali kuona uzembe unaendelea
katika mkoa wetu,lazima watu
wawajibishwe kwa uzembe hasa Kikosi cha
kuzima moto ambao mko karibu na Ofisi
za Chama Cha mapinduzi wilaya yalipo
maduka haya"amesema Mulongo
Chanzo cha moto bado hakijaweza
kufahamika huku maduka hayo yapatayo
188, huku yakiwa hayajaunganishwa na
Umeme kwa lengo la kuepusha hatari ya
moto kwani bidhaa nyingi ni vinyago
vinavyotengenezwa kwa mbao.



LIKE page yetu MJUMBE BLOG facebook au Tutembelee Mtandaoni kwa kuandika MJUMBE BLOG kisha ingia hapo upate picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu kila siku.


©Mjumbe Blog Volunteers

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top