Dk Harrison Mwakyembe
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, jana ilimsulubu
Waziri wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe
ikieleza kuwa wizara yake iliingia mkataba wa
mradi wa treni za kisasa kutoka Stesheni ya Dar
es Salaam hadi Pugu kupitia Uwanja wa Ndege
wa Julius Nyerere (JNIA) bila kufuata taratibu.
Kambi hiyo ililieleza Bunge kuwa mkataba huo
ulisainiwa baina ya mmiliki wa Kampuni ya M/s
Shumoja, Robert Shumake na Shirika la Reli
Tanzania huku Waziri Mwakyembe akishuhudia.
Msemaji Mkuu wa kambi hiyo, Ofisi ya Waziri
Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Pauline Gekul
alitoa madai hayo wakati akiwasilisha maoni ya
kambi hiyo kuhusu muswada wa marekebisho ya
Sheria ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi
(PPP).
Gekul alisema taratibu hazikufuatwa kwa kuwa
haieleweki ni lini Serikali, wakala au Wizara ya
Uchukuzi ilitangaza zabuni ya mradi wa treni
kutoka Stesheni hadi Pugu kupitia JNIA.
LIKE page yetu MJUMBE BLOG facebook au Tutembelee Mtandaoni kwa kuandika MJUMBE BLOG ingia hapo upate picha,Matangazo,Habari mpya,Taarifa muhimu kila mara.
©Mjumbe Blog Volunteers
Post a Comment