Rais kikwete akitoa hotuba yake kwa
taifa .Amesema kuwa amepona saratai ya kibofu.
Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania amesema
amepona saratani baada ya kufanyiwa upasuaji
mapema mwezi huu nchini Marekani.
Kiongozi huyo wa Tanzania mwenye umri wa
miaka 64 ametoa hotuba kwa taifa kuelezea afya
yake..
"Niligundulika kuwa na hatua ya pili ya saratani
ya kibofu, ambayo baadaye ikaonekana kuwa ni
hatua ya kwanza," alisema Kikwete katika hotuba
iliyotangazwa moja kwa moja kupitia televisheni
akiwa uwanja wa ndege wa Dar Es Salaam baada
ya kurejea kutoka Marekani.
Aliongeza kuwa madaktari wamesema sasa hali
yake shwari:
"Madaktari walisema saratani
haikuenea katika sehemu nyingine za mwili na
baada ya upasuaji sasa wamesema nimepona
saratani."
Alisema aligundulika kuwa na saratani ya kibofu
zaid ya mwaka mmoja uliopita na alifanyiwa
upasuaji katika hospitali ya Johns Hopkins
Hospital tarehe nane Novemba.
Kikwete ambaye anamaliza muhula wake wa pili
mwakani amesema wananchi wajenge tabia ya
kupima afya zao ili wagundue maradhi mapema.
LIKE page yetu MJUMBE BLOG facebook ili Ujiunge nasi Katika Kupashana Habari,Kutaarifiana,Picha,Matangazo ya hapa na pale kila siku.
©Mjumbe Blog Volunte
Post a Comment