Jifunze Zaidi;KIU YA MAFANIKIO NA UMUHIMU WA MTU WA MFANO KATIKA NDOTO ZAKO!
Na:Malius Dyanambo
*****************************************************************************************************************************************************************************************************
kipindi fulani mwalimu wa michezo/coach, Dr. Lou Holtz, alisema'' You have got to have great athletes to win, i don't care who the coach is. You can't win without good athletes, but you can lose with them. This is where coaching makes the difference.
AKIWA NA MAANA KUWA: ktk mashindano yoyote, huwezi pata ushindi bila kuwa na wachezaji bora, bila kujali coach anayefundisha wachezaji hawa. Hata hivyo unaweza shindwa mchezo na wachezaji wote walio bora, kama hauna coach bora.
HUU NI UKWELI: maisha ya ushindi ktk taaluma au shughuli yoyote inategemea mambo mawili makuu.
1. MCHEZAJI MWENYEWE: hapa ina maanisha kuwa, mchezaji inabidi awe na bidii na kiu ya kujifunza ili awe bora zaidi kila siku. Ni vigumu coach kumbadilisha na kumfanya mchezaji bora mchezaji yeyote, kama mchezaji huyu hajitumi kuongeza maarifa zaidi kwa lengo la kuwa bora zaidi.
Maisha ya mafanikio yaananzia na mtu mwenyewe kuwa na kiu ya kutaka kutoka alipo/ au kuchukia alivyo leo, na kutaka kusogea mbele kwenye maisha bora.
- kuchukia maisha ya kudharauliwa na watu waliofanikiwa.
- kuchukia maisha ya kuishi mitaa ya uswahilini na miundo mbinu mibovu.
- kuchukia maisha ya kila mwezi kuwaza mambo madogo madogo, na kuwa na wasiwasi vipi utapata chakula, bili za nyumba, watoto vipi wataenda shule, utatoa mchango upi kwa wazazi wako.
- kuchukia kwa nini kundi fulani linazidi kwenda mbele wakati wewe unaendelea kubaki chini....vijana wadogo waliotoka nyuma wanazidi kufanikiwa wakati wewe unaendelea kubaki chini.
- kuchukia maisha ya daladala, wakati magari bora unayoyapenda yako show room yanapigwa vumbi.
CHUKI HII NDIYO INAYOKUFANYA UAMKE MAPEMA NA ULALE UMECHELEWA, CHUKI HII INAKUSABABISHA UWEKE MIPANGO MIKUBWA KILA SIKU NA KUHAKIKISHA MIPANGO HII INAFANYIKA....CHUKI HII NDIYO INASABABISHA WENZAKO MWANZO MLIOKUWA MNAKAA KIJIWE KIMOJA NA KUPOTEZA MUDA WAANZE KUKUCHEKA, NA KUKUITA MPUUZI, MAANA SASA DHAMIRA ULIYONAYO MOYONI HAWAIWEZI KABISA.....CHUKI HII NDIYO INASABABISHA MOTO WA KUTAKA KUONGEZEKA KILA SIKU UENDELEE KUCHOCHEA TUMBONI.....
HAPA NDIPO MWANZO WA MAFANIKIO UNAANZIA!
2. LAKINI HILI UFIKE UNAKOTAKA MAISHANI LAZIMA UWE NA COACH.
au kwa lugha nyingine, uwe na mtu wa karibu ambaye kila siku unapomwitaji anakuwepo ili kukuelekeza jinsi ya kufika huko unakotaka kufika....kimsingi mwalimu huyu sharti awe amefanikiwa kwa kile unachotaka kufanikiwa nacho, aua awe anaendelea kupiga hatua kila siku kuelekea kule wewe unakotaka kuelekea.....TATIZO LINAANZIA HAPA WATU WENGI KUWA NA WAALIMU AMBAO HAWAJAWAHI KUFANYA KILE WATU HAWA WANATAKA KUKUFANYA.
-ni vigumu aliyefanikiwa kwenye biashara ya samaki hakamshauri mtu anayetaka kufanya biashara ya kwenda nje ya nchi.
- ni vigumu shoe shiner kumshauri mtu anayetaka kufanya biashara ya kuuza mkaaa.
- ni vigumu aliyeshindwa katika maisha akakushauri jinsi ya kufanya biashara ya kutoa mafanikio.
- ni vigumu anayefeli katika mitihani kila siku akawa mshauri wa jinsi wewe unavyoweza fanikiwa.
HAPA NDIPO USOMAJI WA VITABU VYA MAFANIKIO UNAPOKUWA WA MSINGI, KUSOMA STORI ZA WATU WALIOFANIKIWA KILE UNACHOTAKA KUFANYA, KUSIKILIZA NA KUANGALIA VIDEO ZA WAO WAMEFANYAJE, WANAENDELEA KUFANYAJE, WAMEPITA VIPI MPAKA WAKAFIKA WALIPO SASA.
HAPA NDIPO MTU HUYU ANAYETAKA KUFANIKIWA UANZA KUTAFUTA MARAFIKI WAPYA....MARAFIKI WENYE KUJUA KILE ANACHOTAKA KUFANYA NA KUFANIKIWA NACHO.....KAMA MWANDISHI MMOJA ALIVYOANDIKA'' kama unataka unataka kuwa mwandishi basi watafute waandishi wa habari, lakini kama unataka kufanikiwa katika tasnia ya uandishi wa habari, basi sharti uwatafute waandishi waliofanikiwa.

Post a Comment