Unknown Unknown Author
Title: RAIS KIKWETE AWAONGEZA MUDA WA UJENZI WA MAABARA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni Mfano wa baadhi ya Maabara nyingi ambazo zimebadilishwa matumizi tu kutoka vyumba vya madarasa na kuviwekea baadhi ya fenicha z...
Pichani ni Mfano wa baadhi ya Maabara nyingi ambazo zimebadilishwa matumizi tu kutoka vyumba vya madarasa na kuviwekea baadhi ya fenicha za kuwekea vifaa vya maabara(Meza na Stuli);Picha na Maktaba ************************************************************************************************************************************************************************************************ Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete ameongeza miezi sita ya kukamilisha ujenzi wa maabara katika shule za sekondari nchini, baada ya muda wa miaka miwili alioutoa awali kumalizika Novemba 30, mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu jana, ilieleza kuwa Rais Kikwete amechukua uamuzi huo ili kuwezesha kazi hiyo inayoendelea nchini kote kufanyika kwa usahihi. Ikulu ilieleza kuwa Rais Kikwete alitoa maelezo hayo Desemba 18, 2014, baada ya kutunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu na Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela iliyopo Arusha, Dk Mohamed Gharib Bilal ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwa mujibu wa Ikulu, kiongozi huyo wa nchi alitumia nafasi hiyo kutangaza kwamba atachangia Sh200 milioni katika Mfuko Maalumu wa Dhamana wa taasisi hiyo ya pekee nchini. Akizungumzia ujenzi wa maabara alisema: “Natoa pongezi za dhati kwa viongozi na wananchi wa Tanzania kwa kazi kubwa na nzuri waliyofanya. Kwa ajili ya kumaliza palipoishia, nawaongezea miezi sita.” Rais Kikwete alisema tathmini inaonyesha kuwa shule 3,463 zinahitaji maabara, zikiwa sawa na vyumba 10,389, lakini hadi Desemba 7, 2014, vilikuwa vimejengwa vyumba 3,867 sawa na asilimia 37.2 ya mahitaji ya vyumba vilivyokamilika. Aliongeza kuwa vyumba 5,891, sawa na asilimia 56.7 viko katika hatua mbalimbali za kukamilishwa, huku 631 sawa na asilimia 6.1 ujenzi wake haujaanza. Alieleza kuwa umuhimu wa kujenga maabara uliongezwa kasi na ongezeko kubwa la shule za sekondari, ambazo zimeongezeka kutoka shule 828 mwaka 2004, hadi kufikia 3, 551 kwa sasa. Hata hivyo, kati ya shule hizo 3,551 ni shule 88 ndizo zilizokuwa na vyumba vitatu kwa ajili ya masomo ya fikizia, kemia na biolojia. Novemba 2012 Rais Kikwete alitoa muda wa miaka miwili hadi Novemba 30 mwaka huu kukamilisha ujenzi wa maabara katika sekondari nchini nzima. Hata hivyo, hadi muda unamalizika, maeneo mbalimbali yalikuwa hayajatimiza agizo hilo. ************************************************************************************************************************************************************************************************

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top