
Fidelis Butahe, Mwananchi
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-
Mageuzi), David Kafulila ameeleza namna
alivyoibua sakata la uchotwaji wa Sh306
bilioni kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow
na kudokeza kuwa kitendo cha baadhi ya
watuhumiwa kugoma kujiuzulu,
kinaonyesha kuna watu zaidi wanahusika.
Kafulila (32), ambaye alikuwa akiulizia
suala hilo kila mara bungeni hadi uamuzi
wa kulijadili ulipofikiwa, amesema
ataendelea kulifuatilia hadi aone mwisho
wake.
Akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) kuhifadhi fedha za malipo
ya tozo ya ufuaji umeme baada ya
Tanesco kuingia kwenye mgogoro na
Kampuni ya IPTL na suala hilo kupelekwa
mahakamani.
Kwa mujibu wa masharti ya uendeshaji
wa akaunti za escrow, fedha hizo
zilitakiwa zitolewe baada ya Mahakama
kutoa uamuzi wa mgogoro huo, lakini
wakati ilitaka pande hizo mbili zikutane na
kukokotoa viwango vya tozo hizo, fedha
hizo zilitolewa na kulipwa kwa mmiliki
mpya wa Kampuni ya Pan African Power
Solutions (PAP), jambo lililosababisha
kuibuka kwa kashfa hiyo.
Akizungumza kwenye mahojiano maalumu
na gazeti hili jana, Kafulila alisema
alilinasa suala hilo kwenye vyombo vya
habari na baadaye kupewa kurasa nne za
maelezo ya sakata hilo, lakini baada ya
kuliingiza kwenye chombo hicho cha
kutunga sheria, wabunge wenzake
waliendelea kumwongezea nyaraka hadi
zikafikia kurasa 604
Post a Comment