
Utafiti mkubwa wa kisayansi umeonyesha kuwa
virusi vinavyosababisha ugonjwa wa Ukimwi vya
HIV, vinapungua makali yake na kushuka kwa
uwezo wake wa maambukizi kwa jinsi
vinavyobadilika.
Watafiti katika chuo kikuu cha Oxford nchini
Uingereza wamefanya ugunduzi huo
walipowafanyia uchunguzi mamia ya wanawake
nchini Botswana.
Kikosi hicho cha madaktari kimegundua kuwa
virusi vya HIV vilikuwa vikiingia katika hatua ya
kuharibu mabadiliko yake ili kuishi na kwa
kufanya hivyo, virusi hivyo kwa sasa vinabadilika
taratibu zaidi na inavichukua muda mrefu zaidi
kusababisha ugonjwa wa UKIMWI kwa watu
wenye kuishi na virusi hivyo.
Wanasayansi hao wamesema kupungua kwa
makali ya virusi vya HIV kutaweza kusaidia
jitihada za kutokomeza virusi hivyo, japokuwa
wameonya kuwa virusi hivyo dhaifu bado ni hatari
kwa afya ya binadamu.
Virusi vya UKIMWI katika mwonekano tofauti
Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Ukimwi
Duniani, Desemba Mosi ya kila mwaka, takwimu
zinaonyesha juhudi zilizofanyika katika
kupambana na ugonjwa huo.
Maambukizi ya virusi vya Ukimwi yameshuka kwa
asilimia 38 tangu mwaka 2001 na idadi ya vifo
vinavyotokana na ugonjwa wa Ukimwi
vimepungua kutoka zaidi ya milioni 2.3 mwaka
2005 hadi milioni 1.5 mwaka 2013.
Haya yakiwa maendeleo mazuri, bado idadi
kubwa ya watu wapatao milioni 35 wanaishi na
virusi vya Ukimwi. Kila siku zaidi ya watu 5,700
wanaambukizwa virusi vya Ukimwi, sawa na watu
karibu 240 kila saa.
Alama ya mapambano dhidi ya UKIMWI
Ifikapo mwaka 2015, watoto milioni 25
watapoteza mzazi mmoja au wote wawili
kutokana na ugonjwa wa UKIMWI.
Ugonjwa huu ni janga kubwa la kijamii duniani.
UKIWMI si tu unawanyang'anya mamilioni ya
watoto maskini kabisa, upendo na ulinzi kutoka
kwa wazazi wao, bali pia watoto wengiwanabakia
kuhangaika peke yao, wengi wakiwa na jukumu la
kuwalea wadogo zao, katika hali ya umaskini
mkubwa, kubaguliwa na unyanyapaa
unaosababishwa na maambukizi ya virusi vya
HIV.
Watoto wengi wanatengwa na mara nyingi ndugu
wa familia zao hawawezi kuwatunza.
Credi
Post a Comment