Unknown Unknown Author
Title: KUHUSU NDEGE YA INDONESIA ILIYOPOTEA LEO;INDONESIA YASITISHA UTAFUTAJI..
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Airasia iliotoweka Indonesia imesitisha utafutaji wa ndege ya AirAsia hadi kesho iliopotea na takriban abiria 160 waliokuwa wakieleke...



Airasia iliotoweka

Indonesia imesitisha utafutaji wa ndege ya AirAsia hadi kesho iliopotea na takriban abiria 160 waliokuwa wakielekea Singapore kutoka mji wa Surabaya nchini Indonesia.

Ndege za kijeshi kutoka indonesia na singapore zilikuwa zikiisaka ndege hiyo kusini magharibi mwa pwani ya Borneo ambapo ndege hiyo ilitoweka.

Takriban abiria 162 walikuwa wakiabiri ndege hiyo aina ya Airbus 320 wengi wao wakiwa raia wa Indonesia.

Ndugu na familia za waathiriwa wa AirAsia wakisubiri habari za kutweka kwa ndege hiyo

Rubani wa chombo hicho anadaiwa kutaka kubadilisha njia ili kuepuka kimbunga lakini hakuomba usaidizi wowote.

Baadhi ya meli katika eneo hilo zinaendelea kuitafuta ndege hiyo,licha ya hali mbaya ya hali ya anga

Familia na marafiki wa waathiriwa wamekongamana nchini Singapore na uwanje wa ndege wa surabaya wakingojea habari kuhusu ndege hiyo.

CHANZO:BBC

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top