Unknown Unknown Author
Title: MZIMU WA MADAKTARI FEKI WAENDELEA KUITESA MOI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Sekta ya afya nchini Tanzania bado inakabiliwa na tatizo la madaktari feki ambapo jana Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa y...

Sekta ya afya nchini Tanzania bado inakabiliwa
na tatizo la madaktari feki ambapo jana Taasisi
ya Tiba ya Mifupa na Upasuaji wa Mishipa ya
Fahamu, MOI ilimkamata daktari feki
aliyefahamika kwa jina la Dismas John Macha
mwenye umri wa miaka 35.
Taasisi hiyo ipo kwenye Hospitali ya Taifa
Muhimbili, MNH jijini Dar es Salaam, ambapo
daktari huyo anadaiwa kujipatia fedha kwa njia ya
udanganyifu kutoka kwa wagonjwa na ndugu wa
wagonjwa kwa madai kwamba angemhudumia
mgonjwa wao.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya
kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo, Mkurugenzi
wa MOI, Athumani Kiloloma, alisema mara ya
kwanza alikamatwa Chuo Kikuu cha Afya na
Sayansi Shirikishi Muhimbili, MUHAS, akijifanya
mwanafunzi wa shahada ya uzamili katika shule
ya tiba.
Dk. Kiloloma alisema alipokamatwa mara ya
kwanza, walitoa matangazo katika hospitali
nzima na kutoa taarifa kwa wananchi, lakini
wanashangaa tukio hilo limejirudia tena.
Akizungumzia tukio hilo, mkurugenzi huyo
alisema wanakabiliwa na tatizo kubwa la
madaktari feki, ambao wamekuwa wakiomba
michango mbalimbali ya fedha.
Mtuhumiwa Dismas Macha anatarajiwa
kufikishwa mahakamani kujibu mashitaka
yanayomkabili.
Awali, Dismas akizungumza na waandishi wa
habari, alisema yeye si daktari bali ni mgonjwa
wa akili. Matukio ya madaktari feki yamekuwa
yakiripotiwa katika hospitali mbalimbali nchini
Tanzania katika siku za karibuni, ambapo
inadaiwa madaktari hao kazi kubwa ni kuwatapeli
wagonjwa na ndugu wa wagonjwa.


©Mjumbe blog Volunteers

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top