AJALI YAUA WAWILI;BEN WA SAA NANE ANUSURIKA KIFO!
Ardhi ni katili,Nimepoteza zawadi...Nimepoteza lulu ya thamani Allan Meshili na Faith.
Ni muda mchache uliopita nilikua nanyi,tukicheka,Kutaniana na kupeana moyo katika ndoto zetu
Allan Patrick Meshili ,Umetangulia.Umeniacha rafiki yako uliyeniahidi utakua nami hadi tone la Mwisho. Umeniachia msiba mkubwa Moyoni.Sijawahi kuwa na Rafiki wa Kweli kushinda kipimo chako Allan.Umetimiza Ahadi yako hadi Pumzi yako ya Mwisho
Faith Makundi,Nilihama siti ya mbele nikahamia kiti cha nyuma ili nisome kitabu ulichoniletea kama zawadi "Banker to the Poor"-Profesa Muhammad Yunus .
Kumbe ilikua ni zaidi ya kubadilishana siti....!
Uliniahidi kutumia likizo yako kuhakikisha kipindi hiki tunapanga na kutekeleza yote tuliyokubaliana hasa proposal yangu ya kutumia VICOBA phasewise na kuanza mchakato wa kutengeneza network kwa ajili ya kuanzisha Benki ya Maendeleo ya Watu wa Rombo.Ulinishawishi nichukue likizo pia kipindi hiki kama wewe na Allan kabla hujarudi Afrika Kusini ili tuweke akili,taaluma na uzoefu wetu pamoja tufanye kazi kwa ajili ya jamii .Tulienda Rombo kwa ajili ya kampeni lakini pia kupata practical experience ya hali ya Rombo
Sasa mmetangulia,bado huko mliko mnataka nichukue Likizo? kwa ajili ya nini sasa?
Sikuamini kama mwisho wetu ungekua hivi,mbele ya Scania ya Mafuta.Aliyetugonga na kukimbia,hajakimbia hukumu bado...!Ni picha za kutisha na kuhuzunisha!
Washirika wangu,watu muhimu katika safari yangu nimewapoteza kwa mkupuo mbele ya Macho yangu.
Sitamkufuru Mwenyezi Mungu,Ana mipango yake.
Ni machozi ya uchungu,Sina wa Kumlilia zaidi yako wewe Mwenyezi Mungu uwalaze pema peponi Allan na Faith
Familia zinahuzunika na kuwalilia.Ni msiba mkubwa kwetu sote
Nahisi Moyo wangu unazimia kwa huzuni.Ni uchungu mkali Moyoni.
Asanteni Makamanda mlioahirisha safari zenu na kuungana nami hadi Muhimbili.Mlinitambua kwa Tshirt ya M4C mkaungana nasi hadi muda huu tunapotoka Muhimbili.Wapo marafiki zangu wa kwenye mitandao #Gabriel na Mkewe #Joyce Mungure.Asanteni sana
Namshukuru Mungu kwa kuniponya katika ajali hii....!Ni wewe pekee Unayejua kwanini umeniponyakatika ajali hii ya tatu katika maisha yangu .Sitakuhoji...!
Kwa leo sina mengi ya kusema.
Mungu awabariki wote mlioungana nasi Muhimbili na marafiki wote mlioko Mbali
Jina la Bwana lihimidiwe !
******************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************************
Ni Maneno ya BEN WA SAA NANE,Kwenye Ukurasa wake wa fb

Post a Comment