Unknown Unknown Author
Title: PICHA ZAIDI YA TANO KUTOKA HAI:SOKO LA SADALA;HIVI NDIVYO ILIVYO KUWA LEO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Naam,Siasa ni Kilimo;Maeneo ya keep Left ya Moshi Arusha.... Taswira kama ilivyo kutoka Soko la Sadala lilipo Wilayani Hai,Moshi Uki...
Naam,Siasa ni Kilimo;Maeneo ya keep Left ya Moshi Arusha....
Taswira kama ilivyo kutoka Soko la Sadala lilipo Wilayani Hai,Moshi
Ukifika Moshi Mjini Ukajichanganya Moja kwa moja na Wenyeji mtaani kuanza kuhemea bidhaa za Nyumbani hasa Kama Matunda,Mboga mboga,Matunda,Viungo mbali mbali,Maziwa,Nafaka,Viazi n.k Unaweza ukaishia Kulalama na kuUONA Mji wa Moshi kama Usio kuwa na chembe hata kidogo ya Kusitiri Masikini na watu wa Kati.Kwani Masoko na wachuuzi wengi walio weka bidhaa katikati ya mji wa moshi na pembezoni bei zao hulenga kukidhi mahitaji ya wakati na hadhi ya Mji.... Unaweza ukajionea tofauti kama utatoka kidogo nje ya mji wa Moshi na Kuelekea Arusha Road,Mpaka Wilayani Hai siku ya Jumamosi utakapo kutana na soko la Bidhaa mbali mbali za shamba zikiwa zina uzwa kwa bei ya kukidhi matamanio ya mwananchi wa kawaida na pilika pilika za hapa na pale Tangu asubuhi mpaka jioni.Ni soko lililo beba matumaini ya wakulima wa Bustani na Wajasiria mali wa wilaya ya hai.Ni Soko lenye pilika pilika zisizo punguza kasi,huku Likiwa Lina Sawili madhari halisi ya Mkoa wa Kilimanjaro,wakazi wake na Sura ya nchi inayo leta matumaini kwa kila mwenye nia na bidii ya kulitumikia Taifa letu na kuongeza kuzo la Uchumi...! Ukifika MOshi, Karibu Hai Siku ya Jumamosi ili Ujifunze jambo na Ujionee tofauti. Kama Mdau mwenza wa MJUMBE BLOG nime jifunza Kuitazama Tanzania kama Inavyo paswa niitazame,Kutokea pale nilipo simama... Pia nimejifunza Kuitazama Nchi yangu Kama ndugu zangu Wa Watanzania Wengine,katika Mazingira mengine wanavyo Itazama.... Pia Nime jifunza kuitazama Nchi yangu TANZANIA;Kama inavyo takiwa itazamwe na Kila awaye yote katika aridhi ya Taifa langu. PIcha na Maelezo Mdau wa MJUMBE BLOG Kilimanjaro,Moshi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top