RIPOTI YA ESCROW IWEKWE HADHARANI;KIKWETE!
Rais Jakaya Kikwete amepokea Ripoti, nyaraka na ushauri wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow na atavifanyia maamuzi wiki moja ijayo.
Rais Kikwete amepokea Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ripoti ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Umma (PAC) na Maazimio ya Bunge kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow.
Baada ya kupokea nyaraka hizo, Rais Kikwete ameelekeza kuwa Ripoti ya CAG iwekwe hadharani kwa ajili ya umma kuweza kuisoma na kujua nini hasa kimesemwa na kupendekezwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali.
Pia ameelekeza kuwa Ripoti hiyo itangazwe kwenye magazeti yanayosomwa na watu wengi na kwenye mitandao ya kijamii, ili Ripoti hiyo iweze kupatikana kwa Watanzania wengi.
Rais Kikwete ameanza kupitia na kusoma nyaraka hizo na katika wiki moja ijayo atazitolea maamuzi kwa maana ya kwamba yale mambo yanayomhusu yeye moja kwa moja atayatolea maamuzi yeye, yale yanayohusu Serikali atayatolea maagizo na maelekezo ya namna ya kuyashughulikia.

Post a Comment