Unknown Unknown Author
Title: TAZAMA PICHA:NILIKUTANA NA AJALI KITONGA,JANA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia. Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa...
Foleni kubwa iliyosababishwa na basi hilo baada ya kuingia mtaroni na kuziba njia. Basi la abiria lenye namba za usajili T 298 BLZ likiwa linatolewa katika mtaro wa Mlima Kitonga mapema leo baada ya kutumbukia. Hali hii imesababisha foleni kubwa kwa magari huku mengine yakishindwa kuendelea na safari zake. Kwa mujibu wa mashuhuda, chanzo cha gari hilo kutumbukia mtaroni ni kufuatia kupata hitilafu na hatimaye uamuzi wa kuliegesha kando ukafanyika kisha abiria wote wakashuka ili kusubiri marekebisho hayo. Haikupita muda mrefu baada ya abiria kushuka gari lilikosa balansi, likaanza kurudi kinyumenyume na kisha kuingia mtaroni. Hakuna mtu aliyefariki dunia wala kujeruhiwa katika ajali hiyo. Picha na MJUMBE BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top