
Ndugu zangu,
Nimemsoma Mwalimu wangu Ndimara
tangu nikiwa Sekondari pale Tambaza. Si
wengi wenye kujua, kuwa Ndimara alipata
kuwa mwandishi wa magazeti ya Chama,
Uhuru na Mzalendo. Nimekutana na
mwalimu wangu Ndimara mara kadhaa,
na kila tunapokutana huwa tunaanzisha
mada ya kubishana kwa hoja.
Na si wengi wenye kujua kuwa Ndimara
alipata kuwa mweka hazina wa NCCR
Mageuzi na hata akawa mbunge kwa
muhula mmoja. Mwalimu wangu Ndimara
anazijua harakati za siasa za upinzani, na
anaifahamu vema media ya nchi hii.
Picha hiyo hapo juu ni ya kwenye
maktaba yangu.
Maelezo na Picha
Maggid,
Iringa.
Tuna shukuru Kwa Kututembelea.
©Mjumbe Blog Volunteer
Post a Comment