Unknown Unknown Author
Title: ACT YATOA TAMKO NA KUWA TENGUA BAADHI YA UTEUZI WAKE!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT- Tanzania, Kadawi Lucas Limbu, kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya AC...

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT- Tanzania, Kadawi Lucas Limbu, kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya ACT-Tanzania, ametengeua uteuzi wa Thomas Matatizo, kuwa mwanasheria wa chama kuanzia leo, tarehe 1 Januari 2015. Mwenyekiti wa ACT-Taifa, amefuta uteuzi huo kwa kutumia ibara ya 37(w) (vi) ya Katiba ya ACT- Tanzania. Bw.Thomas Matatizo ametenguliwa uteuzi wake kutokana na kujipa mamlaka ya kufanya kazi asizotumwa na chama, kushirikiana na wanaokidhoofisha chama na kudhihaki maamuzi halali ya kikao yaliyofanyika jana tarehe 31Desemba 2015 lakini atabaki kuwa mwanachama na mjumbe wa kamati. Katika kikao hicho, Kamati ya watu 11 iliyopewa mamlaka ya kuongoza chama kwa mujibu wa sheria Na. 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, iliamua kumvua uwanachama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT, Samson Mwigamba, Mshauri wa chama Prof. Kitila Mkumbo na wanachama wengine kutenguliwa nafasi walizokabidhiwa kwa nia ya kukieneza chama lakini badala yake wanatumia nafasi hizo vibaya kukigawa na kukihujumu chama. Kwa taarifa hii, tunawaomba umma wa Watanzania kokote waliko, kutosikiliza kauli na vijineno vitakavyotolewa na Bw. Matatizo au Mwigamba. Kauli halali na thabiti ya chama itatolewa na mwenyekiti au yule ambaye amempa mamlaka. Aidha chama chetu hakijampa mamlaka ya kuthibitisha wala kubatilisha maamuzi ya vikao mtu yeyote, bali sheria mama ya chama yaani katiba ndiyo inaelekeza mamlaka yenye uwezo wa kufanya hivyo. _________________________________________________________________________________________________________________________________ Grayson Nyakarungu, Katibu Mwenezi - ACT, Tanzani

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top