Unknown Unknown Author
Title: PICHA ZA MFANO:KUSANYIKO LA UKOO...!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni Kikao cha Ukoo,31 Disemba 2014 Chini ya Kiongozi Langson Ngaya Kiongozi wa Ukoo Mzee Langson Ngaya Katika Ubora wake akihutu...

Pichani ni Kikao cha Ukoo,31 Disemba 2014 Chini ya Kiongozi Langson Ngaya
Kiongozi wa Ukoo Mzee Langson Ngaya Katika Ubora wake akihutubi
Mwenye Koti Jekundu ndiye aliye pewa jina la Babu,Anaitwa Luheji Lakini Kiukoo na Kimila anaitwa Halikumbeye(Jina la babu)
Wana Ukoo wakiwa wanaendelea na Kikao chao cha kiukoo
Nami Nimo....! Na hapa Naruhusiwa Kupiga Picha tu! Naruhusiwa kuchangia hoja yoyote ile,Kma ikisikilizwa na kuhakikiwa na wazee wa ukoo na wana ukoo wanaweza waka ipitisha,Ikawa sehemu ya maazimio yanayo takiwa Kutekelezwa kutoka kikao husika _________________________________________________________________________________________________________________________________ Muundo wa jamii zetu huanzia kwenye hatua ya Familia,Hupitia Ukoo,ili kufikia Taifa na Nchi! Viongozi hawa wa ukoo huwa ni wawakilishi wa Ukoo kwa Kiongozi wa Kimila ndani ya jamii husika.Hili hutegemeana na Utaratibu ulio wekwa ndani ya jamii.Familia inapo ondokewa na baba(ambaye ndiye kiongozi wa awali kabisa kijamii),Huchaguliwa Mtoto wa kiume mkubwa ambaye hupewa JINA la baba,mtoto huyo kuanzia hapo huwa na Mamlaka aliyo kuwa nayo baba kwa kupitia Wazee wa Ukoo ambao humwongoza na kuanza kumshirikisha moja kwa moja kama mjumbe wa familia husika kwenye ukoo huo.Na huyu anaye pewa jina la Baba wa familia,Huwa hapewi KAYA! Kaya husika ni mali ya Wazee wa ukoo wao ile kaya ndipo kwo! Mwenye jina hawezi kusema pale ni kwake,Bali wazee wa Ukoo pale ni kwao. ********************************************************************************************************************************* Tratibu hizi zipo;Ingawa mara kadhaa kama binadamu tume kuwa wepesi kuanza kuzikwepa taratibu hizi na kuzipuuza kwa sababu tuna ziona kama za Kizamani na mara nyingi huwa tuna fanya hivyo ili kukwepa wajibu wetu kwa jamii yetu na kujitengenezea utaratibu wetu nje ya ule wa jamii yetu tunao uona ni rahisi upande wetu.Na wengine hujitoa kwa kusingizia Imani na Dini zao walizo zipokea! Kwani wao wana Amini Viongozi wa Ukoo huchukuliwa na Hujivisha UMUNGU! Ile khali kwa imazi zao wao wana amini yupo MUNGU MMOJA TU,Aitwaye YEHOVA na hapo ndipo huanza kuwa pinga Viongozi wa Kimila.Lakini ili faa waelewa kuwa Viongozi wa Ukoo au wa kimila nao wanaye MUNGU huyu ambaye tuna mwamini.Wao sio akina MUNGU bali wanatekelez wajibu wao kwa kutumia uwezo wa MUNGU ambaye ndiye tuna amini ame wapa mamlaka. _________________________________________________________________________________________________________________________________ Picha na Maelezo Mdau wa MJUMBE BLOG,Zote zilipigwa Mbeya,Mbozi,Isansa(Itumpi)

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top