Unknown Unknown Author
Title: ALICHO KISEMA KAMANDA KOVA KUHUSU PANYA ROAD,KWA MUHTASARI ZAIDI!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kamanda wa Polisi  Suleiman Kova  akizungumza kupitia  TBC 1. Kumekuwa na story jioni ya leo Dar kuhusu kikundi cha watu cha ‘Panya ...
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova akizungumza kupitia TBC 1.
Kumekuwa na story jioni ya leo Dar kuhusu kikundi cha watu cha ‘Panya Road’ kuvamia maeneo mbalimbali, kupora vitu na kupiga watu.
Kamanda wa Polisi Suleiman Kova amezungumza kupitia kituo cha TBC1, amesema kuwa wananchi wanapaswa kuwa na amani kwa kuwa kikundi hicho kina wahalifu wachache, tayari kuwa wawili ambao wamekamatwa na oparesheni inaendelea ili kuwadhibiti.
Sisi kama Jeshi la Polisi tumepata taarifa vilevile kama walivyopata watu wengine, kwamba hao vijana maarufu kwa jina la ‘Panya Road’ walikuwa wamezagaa maeneo mengi…”– Kamanda Kova.
Hawa ni vijana ambao hawana kazi… hawana maadili mazuri… kwanza tuzungumzie uzito wa tatizo, jinsi ambavyo habari zilivyovuma zimevumishwa kubwa zaidi kuliko uzito wa tukio lenyewe… Nataka niwaambie wananchi kwamba endeleeni na shughuli zenu…
Hatukatai kwamba hawa vijana wapo.. lakini nasema suala limekuzwa limetiwa hofu, watu wamepata hofu kupindukia …
Wale wanaopeleka uvumi waache kwa sababu wewe hujaona tukio, ukiletewa message na wewe unampelekea mtu mwingine hiyo sio sahihi…
Tutashughulikia suala la ‘Panya road’ na leo doria inaendelea usiku kucha, wananchi waondoe hofu wajue jeshi la Polisi lipo… Haiwezekani panya road wakatawala Dar es Salaam… Haiwezekani panya road wawe na nguvu kuliko jeshi la Polisi…
Wamekamatwa wawili… tuliwakamata muda mfupi tu baada ya kuanza vurugu zao…”–Kamanda Kova.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top