![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgZq6mOmae7aRfeDfoI7C5pgdRcrAFNFQ5davjSSyRdm9U-3z-XefEUv-zrth3NtLZRl-UDx2GSwQXxx4rztqdR18lkgwP75aD75mCXS98gGbpDNTpr0PveOm7SnYZoSepXq9PvBjVKC4Kj/s640/529169_425894847485982_1240524797_n(1).jpg)
_________________________________________________________________________________________________________________
Askari wa Jeshi la Polisi wilayani Mbozi aliyefahamika kwa jina la Partdick Kondwa (54) mwenye namba D.4176 mwenye cheo cha Sajenti amejiua baada ya kujipiga risasi katika chumba cha vielelezo katika kituo cha Polisi Vwawa wilayani Mbozi mkoani Mbeya.
Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ahmed msangi amesema tukio hilo limetokea saa 9.30 usiku wa kuamkia leo.
Msangi amesema askari huyo alikuwa lindoni, lakini majira ya saa 9.30 usiku aliondoka na kuelekea nyumbani kwake akipitia chumba cha vielelezo ambapo akiwa huko alijipiga risasi na kufa papo hapo.
Kamanda Msangi amesema chanzo cha kifo hicho bado
hakijafahamika na kwamba mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya serikali Vwawa wilayani hapa kwa ajili ya uchunguzi zaidi.
_________________________________________
SOMA ZAID
Askari wa jeshi lapolisi, Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi akiwa katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi mkoani mbeya.
Akizungumza n kwanjia ya simu, kamanda wa polisi mkoawambeya amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na kwamba jeshi lapolisi linaendelea na uchunguzi wa tukiohilo.
Sajenti Patrick mwenye umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake kwenye chumba cha kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya mbozi amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na kuondoka na uhai wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ileje, Rosemary Staki Senyamule.
Baadhi ya waombolezaji ambao wamezungumza na Mwandishi wetu wamesema kuwa wamepokea msiba huo kwa masikitikomakubwa hasa kwa kuzingatia kuwa Sajenti Patrick alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda kazi yake.
Post a Comment