Unknown Unknown Author
Title: KUHUSU:JARIDA LILILOSHAMBULIWA,POLISI LATOA PICHA ZA WASHUKIWA
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wanaume waliokuwa wamejifunika nyuso wamewaua takriban watu 12 katika ofisi za gazeti moja la vibonzo la Charlie Hebdo mjini Paris Ufara...

Wanaume waliokuwa wamejifunika nyuso wamewaua takriban watu 12 katika ofisi za gazeti moja la vibonzo la Charlie Hebdo mjini Paris Ufaransa. Watu wengine saba wameripotiwa kujeruhiwa vibaya. Gazeti hilo lililo mjini Paris limekuwa likilengwa na wanamgambo wa kiislamu siku za nyuma kiasi cha kutoa vitisho vya mauaji kwa mhariri mkuu wa jarida hilo
Jarida la Charlie Hebdo huangazia maswala mbali mbali kw akutumia vibonzo Tukio hilo lilitokea mapema asubuhi wakati watu waliokuwa na silaha walipoingia katika ofisi za gazeti hilo na kuanza kufyatua risasi na kisha wakatoroka kwa gari. Polisi wanafanya msako mkubwa kuwatafuta washambuliaji huku mji wa Paris ukiwa chini ya tahadhari kubwa. Rais wa ufaransa Francois Hollande amelaani shambulizi hilo akisema kuwa nchi hiyo imepatwa na mshangao mkubwa.
_
___ Rais Francois Hollande anasema hana shaka kwamba shambulizi hilo lilikuwa la kigaidi Rais Francois Hollande alisema hapana shaka kwamba shambulizi hilo ni la kigaidi Waandishi wanne wa jarida hilo la vibonzo, akiwemo mhariri mkuu Stephane Charbonnier walikuwa miongoni mwa waliouawa pamoja na maafisa wengine wawili. ***************************************************************************************************** Bwana Charbonnier, mwenye umri wa miaka 47, aliwahi kupokea vitisho vya kuuawa na alikuwa analindwa vikali na polisi. Vyombo vya habari vimewataja wachoraji wengine watatu waliouawa wakiwemo, Cabu, Tignous na Wolinski. Duru zinasema shambulizi hilo lilifanyika wakati wa mkutano wa kila mwezi wa uhariri wa jarida hilo.#BBC ___________________________________________________________________________________________________ Europe Charlie Hebdo kept its line despite threats French magazine targeted in deadly Paris attack is known for controversial cartoons, including ones Three heavily armed men have attacked Charlie Hebdo, a French satirical magazine based in Paris, killing at least 12 people, including four cartoonists and two policemen. Charlie Hebdo spent the past 20 years lampooning public figures in France and Europe, and was also condemned for its controversial cartoons on organised religion. It has drawn repeated threats for its caricatures of the Prophet Muhammad, among other controversial sketches. Al Jazeera's Dominic Kane reports. Source: Al Jazeera

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top