KINA DADA, SHEPU ZA BANDIA NI HATARI KULIKO MFIKIRIAVYO
(Samahani, Picha zinatisha).
Mrembo wa shindano la Miss BumBum la Brazili Bi. Andressa Urach (Miaka 27) ambaye picha zake ziko hapa, ameamua kusaidia ulimwengu kutambua madhara ya "oparesheni za kujiongezea maumbo bandia" (Plastic Surgery).
Mwanadada huyo ambaye ni mshindi wa pili wa shindano hilo kwa mwaka 2012 na ambaye pia ni mtangazaji maarufu wa televisheni aliingiziwa vitu vya bandia katika oparesheni aliyofanyiwa ili awe na makalio makubwa.
Picha hizi zote zinaonesha alivyokuwa amelazwa hospitalini chini ya uangalizi maalum. Mama yake anawaomba wafuasi wake wa twitter zaidi ya 220,000 wamuombee sana.
Mwonekano wa Mrembo huyu katika picha
Pichani Mrembo huyo akiwa katika chumba cha Uangalizi Maalumu
Nasikia hata hapa Tanzania kina dada wanasaka shepu za bandia....sawa endeleeni lakini angalieni yaliyowakuta wenzenu.
Nimeitafsiri kutoka gazeti la daily mail la Uingereza. Nisameheni bure kwa picha.
J. Mtatiro,
DSM.
Ukitaka kujisomea, bonyeza link ifuatayo....
Read more: http://www.dailymail.co.uk/…/Miss-Bum-Bum-contestant-Brazil…
Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook
MJUMBE BLOG
Tuna Omba Radhi Kwa Picha Zote!
Lengo letu ni Kuzitumia Kufundishia Dada Zetu na Wadogo zetu
Wanao IGA KILA WANALO LIFANYA WATU MAARUFU...!
Post a Comment