Unknown Unknown Author
Title: KUHUSU RIPOTI YA KAMATI KUU CHAMA CHA MAPINDUZI... MENGI KUJULIKANA LEO
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe...
Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete (kulia) akizungumza jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu Adam Kimbisa,wakati akitoka nje mara baada ya kumaliza kikao cha kawaida cha Kamati Kuu ya CCM Taifa usiku huu,kilichofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM Kisiwandui Unguja,Zanzibar,kikao hicho kilianza mnamo majira ya saa sita mchana na kumalizika usiku mnamo saa mbili na ushehe hivi huku mambo mbalimbali yakiwa yamejadiliwa ikiwemo suala la sakata la Akaunti ya Escrow,Hali ya kisiasa nchini,uchaguzi Mkuu na mambo ya Maadili na mengineyo.
Pichani ni Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Wanahabari usiku wa kuamkia leo baada ya kikao cha kamati kuu cha CCM kuisha nje ya ukumbi wa Ofisi Kuu ya CCM,Kisiwandui mjini Unguja kisiwani Zanzibar.Nape ameeleza kuwa taarifa rasmi ya yaliyohusu kikao hicho atayaweka wazi mapema leo asubuhi.

Chanzo;Mjengwa blog

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top