Unknown Unknown Author
Title: KWENYE SAGA LA UDOM KUMRADHI KWA PICHA:WENGI WAMIZWA! WAZIRI MKUU OUT! RAIS WA CHUO ASIMAMISHWA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni moja ya wanachuo walio umia wakati wa Maandamano hayo jana walipo amua kuandamana kupaza sauti zao ili kudai fedha ya kujikimu ...

Pichani ni moja ya wanachuo walio umia wakati wa Maandamano hayo jana walipo amua kuandamana kupaza sauti zao ili kudai fedha ya kujikimu


Picha nyingine kijana ambaye jina lake halikujulikana mara moja akiwa ame umizwa vibaya katika tukio hilo.




Hali ilivyo kuwa baada ya waandamanaji kuanza kudhibitiwa na vyombo vya dola,jambo lililo sababisha Taharuki kubwa na kusababisha baadhi ya wanafunzi kuumia vibaya.





Kiongozi wa serikari ya wanafunzi Philipo Mwakibinga ambaye alikuwa waziri mkuu katika serikari ya chuo amefukuzwa chuo moja kwa moja na wakati huo huo rais wa chuo akisimamishwa chuo kwa muda.

Asante ya picha na wadau Mbalimbali

Soma Zaidi....
Na. Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi
Dodoma.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma
inawashikilia wanafunzi 84 wa chuo Kikuu
UDOM kwa tuhuma za kuhamasisha uvunjifu
wa amani Chuoni na kufanya maandamano
haramu kutoka Chuoni kuelekea katika Ofisi
mbalimbali za viongozi wa Serikali zilizopo
Dodoma Mjini leo tarehe 14.01.2015 majira
ya 05:30hrs.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma
Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi
DAVID MISIME – (SACP) ameeleza kuwa
chanzo cha wananfunzi hao wa programu
maalum ya Diploma ya Ualimu kufanya
uhalifu huo ni kikao walichofanya
wananfunzi hao tarehe 13.01.201 wakidai
kuongezewa posho ya chakula na kwamba
hata kiasi ambacho wanapewa wamechelewa
kupewa.
Hata hivyo uongozi wa Chuo uliwaeleza
kuwa wenye mamlaka ya kuzungumzia
swala la kuongezewa posho ni Bodi ya
Mikopo na siyo chuo. Hivyo walitakiwa
kufuata taratibu za kuwasilisha madai yao.
Pia walielezwa kuwa hundi kwa ajili ya
fedha za posho zao zimeshasainiwa na
kuwasilishwa Benki ili waweze kuanza
kupewa posho zao.
Wanafunzi hao hawakuridhika na usiku
wakaanza kuhamasishana kufanya
maandamano jambo ambalo ni kosa kisheria.
Wanafunzi hao wamehojiwa kulingana na
ushahidi ambao umekusanywa na
wamefikishwa mahakamani kwa kosa la
Kufanya Maandamano yasiyo na kibali.
Viongozi waliohamasisha uvunjifu huo wa
sheria baadi wamekamatwa na baadhi
wanaendelea kutafutwa ili nao waweze
kuchukuliwa hatua stahiki. Ushahidi
uliokusanywa unaonyesha jinsi viongozi hao
wameshiriki kuhamasisha kupitia vikao
rasmi na visivyo rasmi, katika vikundi,
kupita katika mabweni na kutuma sms.
Kamanda MISIME ametoa wito kwa
Wanafunzi hao kutumia taratibu
zilizowekwa na Serikali na Chuo kuwasilisha
malalamiko yao ngazi kwa ngazi na siyo
kufanya vitendo vya kuvunja sheria ambavyo
vitawasababishia kukamatwa. Endapo
watafanya hivyo wasije kulaumu mtu kwani
hatua zitachukuliwa kulingana na Sheria
inavyoelekeza ikiwa ni pamoja na
kufikishwa mahakamani.

Tuna shumuru kwa kututembelea!

MJUMBE BLOG Tuna patikana mtansaoni kila mara kwa habari,picha,Matukio,Matangazo na Taarifa muhimu!

Ingia kwa kuandika MJUMBE BLOG.

posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top