Unknown Unknown Author
Title: MAELEZO NA PICHA:KIJUE KIJIJI KILICHO PEMBEZONI MWA NCHI CHENYE UMEME WA BURE! HAKUNA MITA WALA LUKU;WANA ISIKIA TU!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Kwa Mtanzania Ukimwambia kuhusu moja ya kero kubwa anayo kumbana nayo kila kukicha katika maisha yake ya kila siku ni Upatikanaji wa Umeme w...
Kwa Mtanzania Ukimwambia kuhusu moja ya kero kubwa anayo kumbana nayo kila kukicha katika maisha yake ya kila siku ni Upatikanaji wa Umeme wa Uhakika! Wengi wame kaririwa waki lalamikia huduma mbovu wanazo pata kutoka katika shirika la Umeme nchini TANESCO! Umeme umekuwa wa mgao na wenye kukatika katika mara kwa mara ambapo kuna kipindi unaweza ukawa na shughuli ya msingi lakini ukajikuta umeshindwa kuifanya tu kwasabau ya kukatika kwa umeme.Na hapo ukitaka kutumia njia mbadala lazima gharama ya huduma yako ita ongezwa na kuwa mara dufu! Leo MJUMBE BLOG tume amua kuwa letea wadau wetu Kijiji cha Mfano ambacho kwa wanasiasa wange sema kijiji kilichopo pembezoni mwanchi... Ni kijiji chenye hudum a ya Umeme ambayo mtumiaji anahesabiwa gharama kwa kutazama Idadi ya balbu anazo tumia ndani ya nyumba yake.....! Unaweza ukashangaa lakini huo ndio ukweli! Tumia pasi,Tumia jiko la umeme,tumia jokofu ndani ya nyumba yako lakini mwisho wa siku kitakacho hesabiwa ni idadi ya Balbu tu! What a JOY!! Na kila Balbu ni shilingi 4500 kwa mwezi tu.

Pichani juu ni Kijiji cha Mavanga kilichopo mpakani mwa Wilaya ya Ludewa na Ruvuma kama kinavyo onekana
Pichani juu ni Baadhi ya njia za Usafiri zinazo tumika Kijijini hapo kama zilivyo naswa na Kamera ya MJUMBE BLOG
Zao kuu la kilimo kijijini hapo ni Kilimo cha Maharagwe,katika wilaya ya Ludewa Hik ndicho kiini cha Uzalishaji wa Zao hilo
Kijiji kina Mfumo wa maji ya bomba
Jokofu na Majiko ya Umeme hutumiwa na wanakijiji wa Mavanga kama njia ya kurahishisha shughulizao za kila siku na hakuna bili wala kuulizwa maswali na watoa huduma ya umeme huo
Pichani ni soko kuu la mazao katika kijiji cha Mavanga kni soko bora na la kisasa
Naam;Mavanga kuna ofisi za kiserikari pia,seriksri ya jamhuri ya Muungano hii hii unayo ijua wewe! _________________________________________________________________________________________________________________________________________________________ Aliye kwambia UMEME Vijijini ni ndoto nani? Ushahidi huu pichani ni maelezo tosha kuwa Kama wananchi na viongozi wao wata ungana kwa pamoja ina wezekana! Mavanga ni kijiji klichpo mpakani mwa wilaya ya Ludewa na Ruvuma.Ni miongoni mwa Vijiji ambayo serikari na watu wake wanaweza kuvitolea mfano wa kuigwa kwa hatua ambayo wananchi wake wame ifikia.Hatua ya kuwa na Mfumo wa maji ya bomba kijiji kizima,Htua ya kuwa na Soko la uhakika ndani ya kijiji,Hatua ya kuwa na Miundombinu inayo fikika Msimu wote wa mwaka,Hatua ya kuwa na Nyumba bora za makazi ya binadamu! Zaidi ya yote hatua ya kuwa na Umeme wa nguvu za maji wenye uwezo mkubwa Kiasi kwamba umerahisisha baadhi ya shughuli muhimu kwa wananchi wa kijiji na kata hiyo.Ni faraja iliyoje? Mtumishi yupi ambaye atasita kupangiwa kufanya kazi Mavanga Ludewa? Hakika kwa watumishi wanao fanya kazi katika Wialya ya Ludewa Ukiwaambia Utaenda kufanya kazi MAVANGA,Unakuwa ume wapa zawadi ambayo kila mtumishi anaye ishi kijijini angetamani aipate.Zawadi ya maisha bora kwa kila mtanzania. ********************************************************************************************************************************************************* Picha na Maelezo yote Na MTEMBEA BURE ambaye ni Mdau mwenza wa MJUMBE BLOG

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top