Pichani juu ni zile safu za milima ya Livingstone Upande wa pwani ya Matema,Uishio wa vilima ndiko ziwa liliko,Kyela hii!
Safu za vilima vya Livingstone kama vinavyo onekana unapokuwa ulipo mwambao wa pwani ya Ziwa Nyasa,Mkabala na Hospitali ya Kilutheri
Pichani ni Pwani ya Matema,Kyela majira ya asubuhi wenyeji na wavuvi wana wahi ziwani kwenda kusafisha miili yao na wavuvi wana ingia ziwani kwenda kutafuta ridhiki!
Kama unavyo ona pichani kazi ya Uvuvi wa dagaa inaendelea mita chache tu kutoka pwani ya Ziwa!
Naam,Maandalizi ya awali ili kujihakikishia Mitego ipo poa jamaa wana amini hawata kosa mboga uongo kama sio kutimiza malengoo ya kupata kiasi cha kuweza kujikimu,Ni eneo la pwani ya Matema Mkabala kabisa na Mwambao wa Mwalala au kilipo kituo cha kupima VVU Matema
Chombo ionje maji,Na hapo usithubutu kuomba lift! Wazee wa kazi wana ingia kutega mitego yao natamani nami niwape Kampani Lakini MmmH! Na vipi kuhusu kuogelea kama ikitokea Dhoruba? Maana sioni hata Boya moja la Tahadhari ndani ya mitumbwi yao katika maana wote wanao ingia ndani ya chombo hauhitaji kuwafanyia Usaili wa mdomo tena,ni wataalamu walio bobea kwenye kazi yao hawafanyi kwa kubahatisha!
*********************************************************************************************************************************************************
Na wenyeji wa mwambao wa pwani ya Ziwa nyasa watakapo kuambia 'nina wahi ofisini... basi usishangae wana elekea liliko Ziwa na kuingia ndani ya mitumbwi yao!! Ziwa nyasa ni Ofisi yao,Kwani huko ndiko wanako wezesha mikono yao iingie kinywani!! Ofisi sio Jengo! Ofisi ni watu na Shughuli zao za kila siku.
_________________________________________________________________________________________________________________________________________________________
Picha Na
MTEMBEA BURE
Post a Comment