Unknown Unknown Author
Title: TAARIFA:KUHUSU WANACHUO WALIO UAWA NA WALIO UMIA UDOM!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wanafunzi waliokuwa kwenye maandamano ya kudai fedha zao za kujikimu walidai kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wenzao waligongwa na gari ya ...

Wanafunzi waliokuwa kwenye maandamano ya
kudai fedha zao za kujikimu walidai kuwa kuna
baadhi ya wanafunzi wenzao waligongwa na gari
ya polisi iliyokuwa ikitawanya maandamano hayo
ambayo polisi waliyaita ni haramu na kufariki
dunia.
Kufuatia uvumi ulioenea katika mitandao
mbalimbali ya kijamii na katika mji wa Dodoma
na viunga vyake kuwa kuna wanafunzi waliofariki
dunia kufuatia maandamano yaliyofanyika juzi
katika Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom), Mganga
Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa
Dodoma, Dk Nassor Mzee amesema kuwa taarifa
hizo si za kweli.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini
kwake jana mjini hapa, Dk Mzee amesema kuwa
hakuna maiti yoyote ya mwanafunzi wa Chuo
Kikuu cha Dodoma iliyopokelewa katika hospitali
hiyo na kusisitiza kuwa taarifa hizo siyo za kweli.
“Hapa hospitalini hakuna maiti yoyote ya
mwanafunzi wa Udom na hata baada ya kupata
taarifa hizo nilikwenda mapokezi kwa ajili ya
kupata taarifa na kwenye wodi zote hapa
hospitalini lakini hakuna mwanafunzi hata mmoja
wa kutoka Udom aliyefika hapa kutibiwa,”
amesema Dk Mzee.
Aliongeza kuwa, “Hata kwenye chumba cha
kuhifadhia maiti hakuna maiti yoyote ya
mwanafunzi wa udom… labda kama waliamua
kwenda kuzihifadhi maiti hizo kwenye hospitali
nyingine nje ya hapa lakini hapa hakuna maiti
yoyote kutoka Udom.”
Awali baadhi ya wanafunzi waliokuwa kwenye
maandamano ya kudai fedha zao za kujikimu
walidai kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wenzao
waligongwa na gari ya polisi iliyokuwa ikitawanya
maandamano hayo ambayo polisi waliyaita ni
haramu na kufariki dunia.
Pia katika taarifa yake kwa vyombo vya habari
iliyotolewa juzi na jeshi la polisi haikutaja vifo
wala majeruhi zaidi ya kutaja idadi ya wanafunzi
waliotiwa mbaroni kufuatia maandamano hayo
kuwa ni 84.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, David
Misime alisema kuwa wanafunzi wote
waliokamatwa katika maandamano hayo
wameshafikishwa mahakamani kujibu mashtaka
yanayowakabili ya kuvuruga amani chuoni na
kufanya maandamano haramu.


KWA MATUKIO ZAIDI Tutembelee MJUMBE BLOG kila Mara.


Picha hii hapa chini ili tufikia kwa Makosa na Ripota wetu aliye tutumia!!

Taarifa tulizo zipata ni kwamba Kijana huyu pichani aliumia Katika ajali ya pikipiki na sio katika Maandamano ya UDOM juzi.


MJUMBE BLOG tuna omba radhi kwa Usumbufu wowote ule ulio jitokeza.


posted from Bloggeroid

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top