BAADA YA MAUAJI YA CHARLIE HEBDO, PAPA
AMESEMA "UHURU WA HABARI UNA MIPAKA"....
Papa Francis amelaumu kitendo cha
kushambuliwa wafanyakazi wa gazeti la Ufaransa,
shambulizi lililochukua roho za watu 12, lilitokana
na ulipizaji wa kisasi kwa kejeli aliyofanyiwa
Mtume Muhammad. Papa Francis amelaani
mauaji hayo, lakini amesema uhuru wa kutoa
maoni au uhuru wa habari una mipaka - hasa
inapotokea unahusisha dini.
Kwa upekee, Papa amesema, hakuna mtu mwenye
haki ya kutumia uhuru wa habari "kuchokoza" au
"kudhalilisha" watu wengine kimakusudi, na
amesisitiza kuwa wanaofanya uchokozi huo
wasishtuke pale ambapo walioguswa wanachukua
hatua mbaya.
"Hata kama ni rafiki yangu, kama akinitukania
mama yangu, atapata ngumi ya puani. Hiyo ni
kawaida." Amesisitiza Papa Francis.
J. Mtatiro,
Dar Es Salaam,
15 Januari 2015.
(Nimeitafsiri kutoka mtandaoni)
posted from Bloggeroid
Post a Comment