Unknown Unknown Author
Title: BVR ITAENDELEA KUTUMIKA na KUBORESHWA MAPUNGUFU YAKE ILI KUKAMILISHA ZOEZI HILO;PINDA NJOMBE!!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Na Maiko Luoga Njombe Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh, Mizengo Pinda hii leo amezindua rasmi Zoezi la uhakiki wa uandiki...

Na Maiko Luoga Njombe Waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh, Mizengo Pinda hii leo amezindua rasmi Zoezi la uhakiki wa uandikishaji wananchi katika Daftari la kudumu la mpigakura wakati alipokuwa mgeni rasmi katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya polisi vya halmashauri ya mji mdogo wa makambako mkoani Njombe.

Licha ya uzinduzi huo kufanyika hii leo katika mji wa makambako mkoani njombe Tayari zoezi hilo lilianza rasmi February 23 mwaka huu kwa lengo la kuwaandikisha wananchi ambao ndio wapigakura ili waweze kupata haki zao za msingi ikiwa ni pamoja na kuweza kuwachagua viongozi wao wakiwemo wabunge, madiwani na Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ifikapo Mwezi October mwaka huu.

Uzinduzi huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa hapa nchini akiwemo naibu katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA mh, Johnn Mnyika Ambae pia ni mbunge wa Ubungo kupitia chama hicho Nae aliwaasa wananchi kujitokeza ili kuweza kujiandikisha katika daftari la kudumu hukuakisema anaamini kuwa mfumo mpya wa BVR bado ni tatizo kubwa kwa jamii Pia alikuwepo Mwekiti wa zoezi hilo Jaji mstaafu Damiani Lubuva Ambae alitumia nafasi hiyo kuwakumbusha wananchi wa Mkoa wa Njombe kujitokeza kwa wingi katika zoezi la kujiandikisha licha ya kuwepo kwa changamoto mbalimbali katika mfumo mpya wa kutumia mashine za BVR.

Viongozi wengine walio hudhuria uzinduzi huo ni pamoja na Makamu mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM bara Mzee Philip Mangula pamoja na mama tunnu pinda ambaye aliwataka wanawake wa Mkoa wa Njombe kuwa mstari wa Mbele katika kukamilisha zoezi hilo.
 
 ''Ninawaomba wanawake wenzangu msiniangushe muende mkajiandikishe ili muweze kushiriki         kuchagua viongozi mnao wataka katika uchaguzi mkuu mwaka huu kwakuwa wanawake nasisisi tunaweza''  Alisema Mama Tunnu Pinda.

Waziri Pinda alisema kuwa Mfumo mpya wa BVR ni maboresho ya mfumo uliokuwa ukitumika mwanzo hivyo kwasasa mfumo huo utaendelea kutumika licha ya kuwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wananchi wa tanzania na kuongeza kuwa mfumo huo utaendelea kuboreshwa ili uweze kuw na bora na kuweza kukamilisha zoezi hilo.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa wa njombe DKT, Rehema Nchimbi Aliwaeleza wananchi waliojitokeza katika mkutano huo kuwa wakijitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpigakura watakuwa nanafasi kubwa ya kuweza kuwachagua viongozi wanao wataka.




MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kutupa nafasi tukuhudumie,karibu tena.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top