Rais Jakaya Kikwete akipitia kitabu cha
Sera ya Elimu na Mafunzo baada ya
uzindua jijini Dar es Salaam .Picha na
Venance Nestory
Serikali imetangaza Sera ya Elimu na
Mafunzo ya mwaka 2014 inayohuisha na
kufuta sera kadhaa zilizosimamia sekta
hiyo, huku elimu ya msingi ikitakiwa kuwa
ya bure na kuishia kidato cha nne, lakini
wadau wa elimu nchini wana shaka kama
utekelezaji wake utafanyika kwa ufanisi.
Sera hiyo inaweka msingi wa kutatua
matatizo mengi ambayo yamekuwa
yakilalamikiwa na wadau wa elimu
kuanzia ufundishaji hadi maslahi ya
walimu, ikitoa matamko ambayo Serikali
inatakiwa iyatekeleze, mengi katika kipindi
kifupi.
Katika sera hiyo, kutakuwa na mabadiliko
makubwa kwenye mfumo wa elimu ya
awali, msingi na sekondari utakaokuwa
wa muundo wa 1+6+4+2+3+, mfumo
ambao utamaanisha kuwa elimu ya
msingi ambayo itaanzia chekechea hadi
kidato cha nne, itakuwa ni lazima na ya
bure, badala badala ya unaotumika sasa
wa 2+7+4+2+3+, ikimaanisha chekechea ni
miaka miwili, msingi saba, sekondari
minne, elimu ya juu ya sekondari miaka
miwili na elimu ya juu miaka mitatu na
zaidi.
MJUMBE BLOG
Tunakushukuru kwa kutupa nafasi Tukuhudumie!
Karibu tena.
Post a Comment