Mamlaka ya Mawasiliano, TCRA
imeipa leseni ya mawasiliano ya simu
ya mfumo wa 3G kampuni ya Viettel
kutoka Vietnam. Juhudi za kampuni
hiyo zilianza mapema mwanzoni mwa
mwaka huu na tayari imeshaanza
kufanya kazi katika nchi ya jirani,
Msumbiji. Viettel inaingia katika
wakati mgumu zaidi kiushindani katika
biashara ya mawasiliano ya simu,
ukitoa Vodacom, Airtel, Tigo, Zantel
tayari pia kuna mtandao mwingine wa
mawasiliano ulioingia hivi karibuni,
Smart.
Biashara ya Jeshi!
Viettel ni mtandao namba moja nchini
Vietnam na unamilikiwa na jeshi la nchi
hiyo. Kampuni hiyo imekuwa ikijitaidi
kutafuta njia zingine za kukuza mapato
yao kupitia kukuza huduma zao nje ya
Vietnam.
Huduma yote katika mfumo wa 3G
Kampuni hiyo imehaidi kujenga mfumo
wa mawasiliano nchi nzima katika 3G
na sio 2G na EDGE. Hii itasaidia sana
katika kufanya huduma yao ya intaneti
kuwa ya uhakika zaidi kwani bado hadi
leo baadhi ya mitandao mikubwa ya
simu iliyopo inashindwa kutoa huduma
ya uhakika ya 3G katika miji mikubwa
tu nchini.
Ushindani Zaidi katika Biashara Hii
inategemewa Watumiaji ndio
Watakaonufaika Zaidi
Pia wamehaidi kutoa huduma za
intaneti ya broadibandi (broadband)muni
katika mijini na katika miji midogo.
Waziri Msaidizi wa Wizara ya
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia,
Bwana January Makamba alisema ya
kuwa wameitaka kampuni hiyo
isambaze huduma ya fiba (Fibre) katika
hospitali 150 za wilaya, ofisi 150 za
serikali za wilaya, ofisi 65 za posta
pamoja na shule 500 za
sekondari.
TTCL ipo wapi kufanya
haya? Tuambie wazo lako katika hili.
Kwa sasa kampuni hiyo baada ya
kupata leseni hiyo inajikita katika
kutengeneza mifumo yao vizuri na
inategemewa wataanza kutoa huduma
ifikapo Julai mwaka 2015.
MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kututembelea!
Post a Comment