Unknown Unknown Author
Title: MAMA KIKWETE AWATAKA WAKAZI WA LINDI KUIPIGIA KURA YA NDIYO KATIBA PENDEKEZWA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Wananchi wa mkoa wa Lindi wametakiwa kujitokeza kwa wingi kuipigia kura ya ndiyo katiba inayopendekezwa kwani ni bora na imegusa maeneo ...

Wananchi wa mkoa wa Lindi wametakiwa
kujitokeza kwa wingi kuipigia kura ya ndiyo
katiba inayopendekezwa kwani ni bora na
imegusa maeneo yote kwa ajili ya maendeleo ya
Watanzania.
Rai hiyo imetolewa na Mjumbe wa Halmashauri
Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi
(CCM) kupitia wilaya ya Lindi mjini Mama Salma
Kikwete wakati akiongea na wananchi
waliohudhuria sherehe ya kushangilia ushindi wa
uchaguzi wa Serikali za mitaa katika mtaa wa
Ruaha kata ya Mingoyo wilayani humo.
Katika uchaguzi wa Serikali za mitaa, vijiji na
vitongoji uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana
wananchi wa mtaa wa Ruaha waliwachagua
Mwenyekiti na wajumbe wote watano kutoka
Chama Cha Mapinduzi.
Mama Kikwete ambaye ni Mke wa Rais Dkt.
Jakaya Mrisho Kikwete alisema katiba
inayopendekezwa imeangalia maeneo yote
yanayomgusa binadamu ikiwa ni pamoja na haki
za wanawake na watoto, watu wenye mahitaji
maalum wakiwemo walemavu na wazee.
“Katiba iliyopo sasa ilitungwa na baadhi ya watu
waliokuwa madarakani kwa wakati ule na
haikuwahusisha wananchi, lakini hii
inayopendekezwa wananchi wameshiriki kuitunga
kwa kutoa maoni yao”, alisema Mama Kikwete.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Mwantumu Mahiza aliwahimiza wananchi hao
kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga
kura ili wasipoteze haki yao ya msingi ya kupiga
kura.
Mahiza alisema kama kuna watu waliojiandikisha
katika miaka ya nyuma wabebe vitambulisho
vyao ili viweze kunukuliwa na kwa wale wenye
umri wa kuanzia miaka 18 wakajiandikishe na
walio na umri wa chini ya hapo wasijiandikishe.
Aliwaasa wananchi hao kutokubali wageni
waliokaa katika maeneo yao kwa kipindi cha chini
ya miezi sita kujiandikisha.
Akisoma taarifa ya CCM tawi la Ruaha Mohamedi
Ngashona ambaye ni mjumbe alisema viongozi
hao wamejipanga kutatua changamoto
zinazowakabili wananchi wa mtaa huo ambazo ni
uharakishaji wa ujenzi wa zahanati, ukarabati wa
vyumba vya madarasa na ujenzi wa nyumba za
walimu.
Kuwatambua kaya maskini na wazee kwa
kuwapatia huduma muhimu, uimarishaji wa
barabara ya kutoka Mnazimmoja hadi Ruaha na
utekelezaji wa sera ya umeme vijijini hasa
vilivyopitiwa na mradi wa bomba la gesi.
Katika mkutano huo jumla ya wanachama 43
walijiunga na chama hiyo kati yao wanne
walitoka Chama cha Wananchi CUF .
Chanzo:ITV

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top