Unknown Unknown Author
Title: MAHAKAMA IMETUPILIA MBALI PINGAMIZI LA CCM UGOMBEA UENYEKITI WA KIJIJI,MLOWO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Katika uchaguzi wa serikari za mitaa ulio pita Wilayani Mbozi katika kijiji cha Mlowo,aliye kuwa mgombea kwa Tiketi ya CHADEMA aliwekewa pi...

Katika uchaguzi wa serikari za mitaa ulio pita Wilayani Mbozi katika kijiji cha Mlowo,aliye kuwa mgombea kwa Tiketi ya CHADEMA aliwekewa pingamizi kwa kushutumiwa kuwa sio Raia wa Tanzania....!
Hiki hapa ndicho kina endelea:

Na PASCAL HAONGA

Haki inakaribia kushinda dhuluma,leo hakimu
mfawidhi wa Wilaya ya Mbozi ametupilia mbali
pingamizi la CCM lililowekwa dhidi ya kesi
iliyofunguliwa na CHADEMA kijiji cha
Mlowo.Ikumbukwe kwamba CHADEMA kiliweka
zuio la uchaguzi wa nafasi ya MKT kijiji cha Mlowo
kata ya Mlowo wilaya ya Mbozi baada ya ccm
kumuengua mgombea wa CHADEMA kinyemela
wakidai kwamba si raia wa Tanzania bali ni raia
wa Kenya.Pia CHADEMA kilifungua kesi mahakama
ya wilaya ya Mbozi kukitaka ccm kuleta ushahidi
mahakamani unaoonyesha uraia wa Kenya wa Ndg
Willy. Nyamongo(mgombea wa CDM).Pingamizi
lililowekwa na ccm kwenye kesi hii ni kwamba
CDM kilitakiwa kusubiri uchaguzi ufanyike ndipo
wakazuie ushindi wa ccm mahakamani jambo
ambalo lilikuwa gumu kwa makamanda.Leo
mahakama imetupilia mbali pingamizi la ccm na
kesi ya msingi inayowataka ccm kupeleka ushahidi
mahakamani unaoonyesha uraia wa Kenya wa
Willy Nyamongo unasubiriwa tarehe 27/02/
2015.ccm wajiaandae kuleta vielelezo
vinavyoonyesha kwamba mgombea wa CHADEMA
ni Mkenya.Ushindi wa awali umepatikana kwa
CHADEMA.Asante sana wakili msomi Isaya
Mwandi.Tulianza na Mungu,Tunaendelea na
Mungu na tutamaliza na Mungu.



MJUMBE BLOG
Tunakushukuru kwa kutumia huduma zetu.
Asante na karibu tena.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top