Unknown Unknown Author
Title: UWEKEZAJI KATIKA HISA BIASHARA INAYO LIPA HATA MARA MBILI! ZIFAHAMU KAMPUNI ZA HISA ZILIZO FANYA VIZURI 2014!.......
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Ukiwa mwekezaji katika Hisa kuna faida nyingi kama mwekezaji. Moja ni uwekezaji ambao hutakiwi kuwepo katika biashara (pesa yako inakufanyia...
Ukiwa mwekezaji katika Hisa kuna faida nyingi kama mwekezaji. Moja ni uwekezaji ambao hutakiwi kuwepo katika biashara (pesa yako inakufanyia kazi). Mbili pamoja na faida ya ongezeko la bei vile vile unapata gawio kila mwaka au baada ya miezi sita. Vile vile Hisa unazomiliki unaweza kuzitumia kama dhamana unapohitaji mkopo kutoka katika taasisi za fedha.


Kama ungefanya maamuzi ya kununu Hisa kwa mwaka 2014 ungekuwa umepata faida zifuatazo kutoka katika Kampuni hizi ambazo zimefanya vizuri katika soko la Hisa. Bei za Hisa zimepanda mara mbili ukilinganisha na bei ya mwezi wa kwanza (Januari 2014) na bei ya mwezi wa kumi na mbili (Desemba 2014).

Hizi ni Kampuni ambazo bei zimepanda zaidi ya bei ya mwanzo katika Soko la Hisa (DSE). Mfano ungewekeza 100,000 kwa sasa ungekuwa na Hisa zenye thamani ya 180,000 au 190,000 au 200,000 au zaidi.


 Jina la Kampuni
 Bei ya Januari 2 2014
Bei ya Desemba 31 2014
 Kiasi kilicho ongezeka
 Ongezeko kwa asilimia (%)
Tanzania Cigarette Co. (TCC)
 8,600
 16, 740
 8,140
 94.6%
 Swissport Tanzania Ltd
 2, 680
 5, 010
2, 330
 86.9%
 TOL Gases Ltd
     310
     550
    240
 77.4%
 Tanzania Breweries Ltd
 8,000
14, 090
6, 090
76.1%
 Jubilee Holdings Ltd
 5, 120
  8, 510
 3, 390
 66.2%
 CRDB Bank
     280
      430
     150 
 53.6%
 DCB  Commercial Bank
     490
      720
     230        
 46.9%
 Acacia Mining Plc (Barick)
 4, 860
  6, 810
 1, 950
 40.1%









 Kama ungefanya uwekezaji Januari 2014 basi ungenufaika na ongezeko la bei ya Hisa kwa Kampuni ambazo zimeonyeshwa hapo juu.


Kwa mwekezaji ambaye angenunua Hisa za kampuni ya TCC angepata ongezeko la asilimia 94.6% kwa mwaka mmoja. Kwa kila Hisa ambayo amenunua kwa mwezi Jauari 2014 kufika Desemba 2014 alikuwa na ongezeko/faida ya Shilingi ya Kitanzania Tshs. 8,140. Ungeweka pesa yako Benki ungepata riba ya asilimia 4% au 5% au 7% kwa mwaka mzima.

Ila Soko la Hisa la Dar es Salaam linakupa fursa ya kuwa mmiliki wa kampuni huku ukinufaika na ongezeko la bei pamoja na gawio la faida ambayao kampuni itapata kwa mwaka au baada ya miezi sita.

Jinsi gani inaonyesha kuwa kuna fursa kubwa katika uwekezaji katika Hisa na ukaweza kutengeneza faida katika Husa huku ukiwa unaendelea shughuli zako nyingine.

"Wekeza Inalipa" 

Kwa Ushauri kuhusu kuwekeza katika Hisa 
emmanuelamahundi@gmail.com au +255714 445510



MJUMBE BLOG
Tunashukuru kwa kutupa fursa tukuhudumie mtandaoni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top