Mbunge wa Monduli ,Edward Lowassa akiagana na Masheikh wa wailayani Bagamoyo mkoani Pwani baada ya kumkabidhi mchango wa kuchukua fomu ya kuwania urais nyumbani kwake,Dodoma jana.
Hatimaye mbunge wa Monduli, Edward Lowassa amesema "ameshawishika" na kuweka bayana kuwa atachukua fomu ya kugombea urais kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Lowassa, ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya Awamu ya Nne, amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja wa makada wa CCM wanaowania urais, lakini hakuwahi kutangaza nia ya kuwania nafasi hiyo ya juu ya uongozi nchini.
Lakini jana, alilazimika kufunguka kuhusu suala la urais ambalo lilimfanya yeye na wenzake watano wafungiwe kwa kipindi cha miezi 12 kujihusisha na harakati hizo baada ya Kamati Kuu ya CCM kuwatia hatiani kuwa walianza kampeni mapema kabla ya muda kufika.
Credit:Mjengwa
MJUMBE BLOG
Tuna shukuru kwa kutupa fursa tukuhudumie.
Post a Comment