Unknown Unknown Author
Title: PIGO KWA CCM, NI NANI ATAIMBA KAMA KOMBA?
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
JOHN  DAMIANO KOMBA 1954        Alizaliwa 1963-70   Shule ya Msingi Lituhi 1971-74   Shule ya Wavulana Songea 1975-76   Chuo ...

JOHN  DAMIANO KOMBA 1954        Alizaliwa 1963-70   Shule ya Msingi Lituhi 1971-74   Shule ya Wavulana Songea 1975-76   Chuo cha Ualimu Kleruu 1988-90   Chuo cha Magdeburg path 1978-79   Chuo cha Kijeshi Monduli 1978-92    Ofisa wa JWTZ 2006-08    Chuo Kikuu cha Washington 2005-15    Mbunge Mbinga Magharibi  

Mbunge wa Mbinga Magharibi na mkurugenzi wa kundi la uhamasishaji la CCM, Tanzania One Theatre (TOT), Kapteni mstaafu John Komba (61), amefariki dunia jana.
Akithibitisha kifo hicho Dk Elisha Ishan alisema; “Nilimpokea na kuanza kumpima shinikizo la damu na vipimo vingine lakini tayari vilikuwa havifanyi kazi na hapo ndipo tukathibitisha kuwa ndugu yetu ameaga dunia.”
Dk Ishan wa Hospitali ya TMJ alisema kuwa, Kapteni Komba  alifikishwa hospitalini hapo saa 10:00 jioni akiwa amebebwa katika machela.
Dk Ishan alisema hawezi kujua kilichomuua lakini akaongeza alikuwa na tatizo la shinikizo la damu na hivi karibuni alikwenda kwenye kiliniki yake.
“Kwa kifupi ni hayo na kwa sasa mwili wake umepelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo.”
Akizungumzia msiba huo, Mkurugenzi wa Idara ya Shughuli za Bunge, John Joel alisema Komba aliyekuwa nyumbani kwake Tangi Bovu jijini Dar es Salaam alianza kujisikia vibaya kutokana sukari yake kuwa juu wakati huo huo presha yake nayo ilikuwa imepanda, hivyo walimpeleka Hospitali ya TMJ iliyopo Upanga kwa matibabu.
Alisema kwa sasa mwili wa mbunge huyo ambaye ni kada wa maarufu wa CCM umehifadhiwa Hospitali ya  Lugalo na kwamba taratibu za mazishi zinaendelea nyumbani kwake.
Nape amzungumzia
Awali Katibu wa Nec, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Nape Nnauye alisema kuwa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho imepokea kwa mshituko taarifa ya kifo hicho  iliyotokea ghafla.
“Pengo lake ni vigumu kuzibika nikinukuu maneno ya Mwenyekiti wa chama chetu Taifa, Jakaya Kikwete; “ Chama kimepata pigo kubwa ukizingatia kwamba alikuwa kada na mhamasishaji mkubwa wa chama na kwamba atabaki kuwa historia iliyotukuka.”
Mtoto wake asimulia
Mtoto wa marehemu, Claudia alisimulia kifo cha baba yake kuwa: “Baba alianza kujihisi vibaya wiki iliyopita na walimpeleka Hospitali ya Sanital, Mikocheni na alionekana  shinikizo la damu na sukari vipo juu.”
CHANZO:MWANANCHI LEO

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top