![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEguOWaSpaVHJm6bscK18Wilpd6BoPg0EEW7BRqWM9MGHMqqBniCLkwa51o2XvwsuCYV-Uy9dNuBRRoA2sPE8kcr6UCTGpi8Y8ZKXZ4v_xNONHIsDOTFh4tLNfCcdAjVpLZR4WfVgV8kDEQe/s640/1430452308077.jpeg)
TIMU zaidi ya 50 zinatarajia kupambana katika kuwania kitita cha shilingi Milioni moja katika ligi ya mpira wa miguu Jiji la Mbeya itakayoanza kutimua vumbi Mei mosi mwaka huu katika viwanja tofauti.
Akizungumza na vyombo vya habari katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa Sokoine, Afisa uhusiano wa Ligi hiyo, Rashid Abdalah, alisema ligi hiyo itajilikana kwa jina la Kajuna cup 2015 kutokana na kufadhiliwa na Mwenyekiti wa Umoja wa vijana Mkoa wa Mbeya, Aman Kajuna.
Alisema lengo la kuanzisha ligi hiyo ni kuibua vipaji kwa wakazi wa Mbeya ili baadaye ipatikane timu nyingine ambayo inaweza kuungana na timu za Tanzania Prison na Mbeya city katika ligi kuu Tanzania bara.
Abdalah alisema ligi hiyo itaendeshwa kwa mtindo wa mtoano ambayo itachezwa katika viwanja vinne tofauti ambavyo ni uwanja wa Uyole, Shule ya Msingi Mwege, shule ya msingi Ruandanzovwe na uwanja wa Shule ya msingi Mbata.
Alisema timu zitakazoshiriki ligi hiyo zitanunua fomu maalumu ambayo itauzwa kwa shilingi 30,000, fomu ambazo zitaambatanishwa na kanuni mbali mbali zitakazosaidia kuendesha ligi pasipokuwa na misuguano yoyote.
Alizitaja zawadi ambazo washindi watazipata kuwa ni kila kiwanja kitatoa msindi mmoja ambaye atapata zawadi lakini Mshindi wa jumla wa kwanza atajipatia shilingi Milioni moja, Mshindi wa pili shilingi laki tano na timu.
MJUMBE BLOG
Ni Ukurasa wa Habari,Picha,Matukio,Matangazo.
#KUJERUHI hisia za watu/mtu si Kusudi letu.
MAONI PIGA:0752025002
Post a Comment