Wakati uchaguzi mkuu wa Shirikisho la soka dunia FIFA ukitarajiwa kufanyika keshokutwa, leo kuna taarifa mpya kutoka ndani ya shirikisho hilo.
Kumekuwa na malalamiko mengi kutoka kwa mashabiki wa soka duniani ambao wamekuwa wakilalamikia utendaji mbovu wa viongozi walioko madarakani na hadi kupelekea wagombea waliokuwa wakiwania nafasi ya Urais ndani ya Shirikisho hilo kuamua kujindoa.
Makamu wa Rais wa FIFA Jeffrey Webb
Taarifa mpya zinadai kukamatwa kwa tuhuma za rushwa kwa maafisa sita wa Shirikisho hilo wakiwa katika hoteli moja ya kifahari mjini Zurich, Switzerland.
Maafisa hao ni pamoja na makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb na wanashikiliwa wakisubiri kupelekwa Marekani kwa ajili ya uchunguzi huku Rais Blatter naye akiwa mmoja wa washtakiwa wlaiokuwa wakichunguzwa kwa muda mrefu lakini hayupo kwenye orodha ya waliokamatwa.
Maofisa hao wakiingia ndani ya gari la polisi huku wakiwa wamejifunika wasipigwe picha na waandishi wa habari
Shutuma hizo zinahusisha rushwa ya kiasi cha dola milioni 150 kwa kipindi cha miaka 20 ambazo zilikuwa zikichunguzwa na wapepelezi kutoka Marekani.
Wanachama wa Fifa watakutana mjini Zurich kwa ajili ya mkutano wao wa mwaka siku ya ijumaa wakati rais wa Shirikisho hilo Sepp Blatter akiwa anawania nafasi hiyo kwa muhula wa tano akiwa amebaki peke yake.
Msemaji wa FIFA, Walter de Gregorio amesema licha ya maofisa hao kutiwa mbaroni, maandalizi ya uchaguzi wa Rais wa Fifa yataendelea kama kawaidaCHANZO.MILARD AYO
Post a Comment