Unknown Unknown Author
Title: TASWIRA PICHANI SIDO HALISI HII:VIWANDA VYETU TANGU ZAMA ZA MAWE MPAKA CHUMA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Pichani ni Taswira kutoka kijijini! Katika picha zote ni ishara ya kumbukumbu sahihi ya kimaendeleo aliyo pitia mwanadamu ambayo katika ...

Pichani ni Taswira kutoka kijijini!


Katika picha zote ni ishara ya kumbukumbu sahihi ya kimaendeleo aliyo pitia mwanadamu ambayo katika hayo baadhi ya jamii ime yapitia na kila hatua ili kua bora kuliko iliyo tangulia!

Hapa kuna zama za mawe na zama za chuma pia!

UFAFANUZI:
1.Picha ya kwanza juu ni jiwe linalo itwa "ULWALA";
Jiwe hilo ni hatua moja wapo kubwa ya kimaendeleo aliyo ifikia mwanadamu.

'Lwala' kwa leo ni sawa na mashine za kisasa za kusagia nafaka! Ili kupata Unga.
Mfano:Uwele,Ulezi na Mtama uliweza kusagwa hapo ili kupata unga.

2.Picha ya Kushoto chini " KINU NA MCHI";
au 'MORTAR and PESTLE' kama inavyo julikana kwenye rejea nyingi za kihistoria.
Hiki pia ni kama kiwanda cha kukoboa nafaka na kusindika pia.
Mfano:Mpunga ulikobolewa kwa kutumia Mchi na Kitu,Mahindi,Karanga,Mbura,Dawa,
Mboga mwitu,Mihogo,Ulezi, n.k
Tofauti na zama za leo kuna mashine rasmi ya kukoboa kila aina ya nafaka;jamii ya kale iliyo endelea vema ili pitia katika hatua ya kutumia dhana hizi.


3.Picha ya kulia "MBOGOLO" au 'FURNANCE';
Unapo ongelea dhana za chuma!
Ni maendeleo makubwa aliyo yafanya binadamu katika zama za maisha yake.
Kuna taarifa za kihistiria kuwa watu wa kwanza kutumia chuma na kukisambaza zaidi ni WABANTU;Hawa ina aminika walitokea Kameruni(kasikazini mwa Afrika),Waka pitia Afrika ya kati,Kisha Afrika Mashariki na Kuelekea Kusini mwa Afrika! Sehemu zote walizo pitia walieneza uhunzi pia.

Kiwanda hicho unacho kiona pichani ni cha kufua chuma!
Japo kime boreshwa zaidi ili kuongeza ufanisi na Urahisi wa kazi.Tofauti na zamani ilipo kuwa unavukiza moto kwa hewa iliyo kusanywa kwenye ngozi ambayo ime unganishwa na chuma!
Leo pale Kisangani,Mkiu_Ludewa wanatumia dhana bora zaidi.

Naaam;
Mbio zetu tangia uhuru,mpaka tulipo fika leo ni umbali mrefu!
TUME TOKA MBALI....
Pia tunako elekea ni mbali mno!

Tufanye kazi kwa bidii na maarifa!
Kwani kazi ndicho kipimo cha maisha.


CREDIT:PICHA NA MTEMBEA BURE!

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top