Unknown Unknown Author
Title: KAMPENI ZA KUTOKOMEZA FISTULA ZAINGIA KIBONDO!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Balozi wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba” akitoa elimu kwa wakazi wa Kibondo kuhusiana na maradhi ya fistu...

Balozi wa maradhi ya Fistula nchini Msanii Mrisho Mpoto alimaarufu”Mjomba” akitoa elimu kwa wakazi wa Kibondo kuhusiana na maradhi ya fistula na kuwasihi wakina baba kuwaruhusu wake zao wakatibiwe maradhi hayo kwani yanatibika. Alitoa elimu hiyo wakati wa kampeni inayoendeshwa na Vodacom Foundation kwa kushirikiana na CCBRT ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea katika mikoa mitatu nchini. Inakadiriwa wastani wa wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wanapojifungua.


Wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Kumwamba iliyopo Wilaya ya Kibondo Mkoa wa Kigoma walijumwika na wakazi wa wilaya hiyo katika viwanja vya Community Centre wakimsiliza Meneja Biashara wa Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Grace Lyon wakati alipokuwa akiwafafanulia jambo kuhusiana na maradhi ya Fistula. Wakati wa kampeni ya kutokomeza maradhi hayo inayoendelea kufanyika katika mikoa mitatu nchini,Kampeni hiyo inaendeshwa na Hospitali ya CCRBT kwa kushirikiana na Vodacom Foundation. Inakadiriwa wastani ya wanawake 3,000 hupatwa na maradhi hayo kwa mwaka wakati wa kujifungua.
Cresit:Michuzi

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top