UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA UNASIKITIKA KUWATAARIFU ABIRIA WA TRENI YA DELUXE YA KWENDA KIGOMA LEO JUMAPILI MEI 31, 2015, KUWA SAFARI HIYO IMEAHIRISHWA HADI KESHO JUMATATU SAA MBILI USIKU!
TAARIFA HIYO IMEELEZA KUWA SABABU ZA KUAHIRISHWA SAFARI HIYO NI AJALI YA TRENI YA MIZIGO ILIYOTOKEA JANA SAA 2 USIKU KATIKA STESHENI YA SARANDA AMBAPO MABEHEWA 4 YAMEPINDUKA ! TAYARI WAHANDISI NA MAFUNDI WA TRL WANAELEKEA ENEO LA KWA KAZI YA KUYAINUA NA PIA KUKARABATI NJIA!
ATAYESOMA TAARIFA HII AMUARIFU NA MWENZAKE!
UONGOZI WA TRL UNASIKITIKA KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA!
IMETOLEWA NA AFISI YA UHUSIANO KWA NIABA YA KAIMU MKURUGENZI MTENDAJI MHANDISI ELIAS MSHANA
DAR ES SALAAM
MEI 31 , 2015
Post a Comment