Unknown Unknown Author
Title: SEPP BLATTER:APENYEZA KILELENI KWA KURA URAIS FIFA TENA!
Author: Unknown
Rating 5 of 5 Des:
Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Sepp Blatter leo amefanikiwa kuchaguliwa kushika tena wazifa huo katika uchaguzi mkuu uliofany...

Rais wa shirikisho la mpira wa miguu duniani Sepp Blatter leo amefanikiwa kuchaguliwa kushika tena wazifa huo katika uchaguzi mkuu uliofanyika Zurich nchini Uswisi.

Blatter amefanikiwa kushika tena wazifa huo baada ya kupata kura 133 katika raundi ya kwanza na Prince Ali akapata kura 73.
 Kwa kuwa Blatter hakupata nusu ya kura zote (140), uchaguzi ulielekezwa katika raundi ya pili, lakini mpinzani wake Prince Ali akajitoa.  Maana yake, babu wa umri wa miaka 79, Blatter ataendelea kuongoza soka duniani kwa awamu ya tano.  

Blatter ameshinda uchaguzi huo kiume haswa, kwani alikuwa anapigwa vita kubwa na nchi za Ulaya chini ya Shirikisho lake, UEFA wakiongozwa na Uingereza. Kuelekea uchaguzi huu, kashfa nyingi ziliibuliwa ikiwemo ya rushwa ya Pauni Milioni 100, ambayo Wazungu waliishikia bango wakitaka Blatter aachie ngazi. 

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top